Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Mitandao ya intaneti kwenye ngazi ya jamii ndio jawabu la kufikisha teknolojia kwa walio pembezoni- Bi. Lugangira

Mitandao ya intaneti kwenye ngazi ya jamii ndio jawabu la kufikisha teknolojia kwa walio pembezoni- Bi. Lugangira

Pakua

Mkutano wa 67 wa Kamisheni ya hali ya wanawake duniani, CSW67 ukiendelea na maudhui makuu yakiwa ni namna ugunduzi na teknolojia ya dijitali inaweza kuchangia kumkwamua mwanamke, Idhaa ya Kiswahili  ya Umoja wa Mataifa nayo inaendelea kuzungumza na washiriki ili kufahamu kule watokako hali iko namna gani na nini kinafanyika ili kuhakikisha teknolojia ya kidijitali inatumika kivitendo badala ya kusalia kwenye makabrasha au kumilikiwa na wachache na hivyo kuzidi kuongeza pengo la kidijitali. 

Miongoni mwa washirii ambao Idhaa hii imezungumza nao ni Neema Lugangira, mbunge wa Chama Cha Mapinduzi, CCM, nchini Tanzania akiwakilisha mashirika yasiyo ya kiserikali. Katika mahojiano yake na Flora Nducha wa Idhaa  ya Kiswahili ya Umoja wa Mataifa, Bi. Lugangira amezungumzia ni kwa kiwango gani teknolojia ya  kidijitali inatumika Bungeni na zaidi ya yote mikakati yake ya kuona intaneti inafikia wengi walio pembezeno. Lakini kwanza anamulika matumizi ya teknolojia kwa ujumla wake nchini Tanzania. 

Audio Credit
Selina Jerobon/Flora Nducha
Audio Duration
4'40"
Photo Credit
UN News