Chuja:

NEEMA LUGANGIRA

UN News

Mahojiano la Mbunge Neema Lugangira wa Tanzania kuhusu nafasi ya mbunge kwa umma

Uwepo wa wabunge wenye nguvu ni msingi imara wa Demokrasia kwa mujibu wa lengo namba 16 la malengo ya maendeleo endelevu, SDGs ya Umoja wa Mataifa linalolenga amani, haki na taasisi thabiti. Hilo ni dhahiri kwa kuwa wawakilishi hao wa wananchi wanakuwa na uwezo wa kutunga sheria, kutenga fedha kwenda kufanya kazi ya utekelezaji wa sheria na sera walizozipitisha na kuwajibisha serikali iwapo haijatenda yale wananchi wanayakusudia kwa kuzingatia makundi yote kwenye jamii hususan walioko kwenye mazingira magumu. 

Kuelekea siku ya kimataifa ya Mabunge 30 Juni, Leah Mushi amefanya mahojiano na mbunge wa Bunge la Jamhuri wa Muungano wa Tanzania, kuhusu nafasi ya wabunge katika kuhakikisha usalama wa wananchi wao hususani wakati huu dunia ikipambana na janga la corona au COVID19. kwanza anaanza kwa kujitambulisha 

Sauti
8'51"

JUNI 28 2021

Uchambuzi wa habari zetu hii leo ambapo kuelekea siku ya mabunge duniani juni 30 tutakuletea mahojiano maalum na mbunge wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Neema Lugangira kuhusu nafasi ya bunge kwa umma ikiwemo kuelimisha kuhusu mapambano ya Janga la CORONA. 

Pia utasikia habari kwa ufupi ambapo Flora Nducha atakujuza kuhusu ripoti ya UNODC, ubaguzi wa kimfumo na angalizo la WHO kuhusu akili bandia kwa afya.