Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Hofu ya athari yatanda huku kimbunga Freddy chabisha hodi Msumbiji: WMO

Hofu ya athari yatanda huku kimbunga Freddy chabisha hodi Msumbiji: WMO

Pakua

Kimbunga Freddy moja ya vimbunga vilivyodumu kwa muda mrefu na kusababisha athari kubwa sehemu mbalimbali sasa kimeondoka Madagascar na kubisha hidi Msumbiji ambako kwa mujibu wa shirika la Umoja wa Mataifa la utabiri wa hali ya hewa duniani WMO kinaleta tishio kubwa kwa sababu ya kiwango cha mvua kinachoambatana nacho.

WMO inasema kimbunga Freddy kimeshika kasi kwenye mkondo wa Msumbiji kikitokea Madagascar huku kikiambatana na upepo mkali na mvua na kinatarajiwa kupiga kikamilifu Msumbiji mchana wa leo Ijumaa Machi 24 na uwezekano mkubwa ni katika maeneo kati ya Beira na Inhambane. 

Hata hivyo shirika hilo la utabiri wa hali ya hewa limesema tahadhari za mapema na hatua zilizochukuliwa mapema zimesaidia kudhibiti idadi ya vifo hasa Madagascar na sasa Msumbiji hali ambayo inadhihirisha umuhimu wa kampeni inayoendelea kote duniani ya kuhakikisha tahadhari ya mapema inatolewa kwa wote. 

Ofisi ya Umoja wa Mataifa ya kuratibu masuala ya kibinadamu na misaada ya dharura OCHA imeonya kwamba “tishio la kimbunga hicho litasababisha janga kubwa la kibinadamu nchini Msumbiji.” 

Taasisi ya kitaifa ya kudhibiti majanga Msumbiji inakadiria kwamba mafuriko makubwa katikati na Kusini mwa Msumbiji kutokana na kimbunga hicho yanaweza kuathiri hadi watu milioni 1.75. 

Hatari kubwa ya kimbunga Freddy Msumbiji imeelezwa kuwa uwezekano mkubwa wa mvua kubwa inayopaswa kunyeksha kwa muda wa mwezi mmoja kunyesha kwa siku kadhaa na hivyo kusababisha mafuriko katika taifa ambalo tayari udongo wake umejaa maji na mito imefurika kutokana na msimu wa mvua usiotarajiwa.
WMO inasema kimbunga Freddy ni cha aina yake kwa sababu ya umbali kinachoweza kusafiri na muda kinachoweza kudumu.  

Kilianza Februari 6 kwenye mwambao wa Kaskazini Magharibi mwa Australia na kuathiri mataifa kadfhaa ya visiwani ikiwemo Mauritius na Réunion, wakati wa safari yake ndefu kupitia Kusini mwa bahari ya Hindi nah ii ni nadra sana linasema shirika hilo kwani kimbunga cha karibuni cha aina hiyo kilichorekodiwa ni Leon-Eline na Huda vyote vilitokea mwaka 2000. 

Audio Credit
Flora Nducha
Audio Duration
2'15"
Photo Credit
© UNICEF/Claudio Fauvrelle