Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Asante TANBAT 6 kwa ushirikiano, wasema viongozi wa Mambéré-Kadéï

Asante TANBAT 6 kwa ushirikiano, wasema viongozi wa Mambéré-Kadéï

Pakua

Viongozi wa eneo la utawala la Mambéré-Kadéï nchini Jamhuri ya Afrika ya Kati, CAR wamewashukuru viongozi wa walinda amani wa Umoja wa Mataifa kutoka Tanzania wanaohudumu chini ya ujumbe wa Umoja wa Mataifa wa kulinda amani nchini humo, MINUSCA katika eneo hilo la Berbérati kwa kutambua kuwa ulinzi wa amani unategemea ushirikiano wa wageni na wenyeji.

Shukrani za viongozi wa mkoa wa mkoa wa Mambéré-Kadéï na wilaya ya Berbérati ambako ndiko hasa makao makuu ya kikosi cha 6 kutoka Tanzania kinacholinda amani kupitia Umoja wa Mataifa, zinakuja baada ya mara kwa mara kikosi hiki licha ya kulinda amani lakini pia kimekuwa kikishirikiana na viongozi wa kijamii ili kujua changamoto zinazowakabili ili kutafuta namna ya kuzitatua kwa kuzingatia mahitaji ya jamii yenyewe. Mkuu wa Mkoa wa Mambere Kadei, Kanali Magengegue anawasilisha salamu hizo kwa Luteni Kanali Amani Mshana ambaye ni Mkuu wa TANBAT 6 baada ya ziara ya kikosi hicho ofisini kwake, "Tanzania na wanajeshi wake wana upendo sana kwetu sisi ni kama dada au kaka au mama na hata baba kuja kwako mkuu wa kikosi kunitembelea kama ziara yako kwangu  ni ishara tosha kwetu kwa undugu wetu namimi ninaahidi ushirikiano huu kudumisha kama ilivyokuwa kwa vikundi vilivyopita kutoka Tanzania.”   

Naye Mkuu wa wilaya ya Berberati ambayo ni mwenyeji wa kikosi hiki cha Tanzania akawa na haya ya kusema,  "Tangu kikundi hiki kimefika kwakweli kimeonesha kasi kubwa katika ushirikiano wa karibu na wananchi wangu ninaowaomgoza hapa Mambele Kadei. Tumeshudia mkitoa matibabu, dawa na hata elimu za ujasiliamali kwa wanawake na vijana Ili wajipatie kipato na kuepuka kuingia katika vikundi vyenye nia mbaya na serikali hii ni ishara tosha kwetu kuwa walinda amani  kutoka Tanzania chini ya Umoja wa Mataifa wanafanya kazi kuwa yenye tija kwetu tangu waanze  jukumu la ulinzi wa amani. Nina furaha sana.” 

Audio Credit
Kapteni Mwijage Francis Inyoma
Audio Duration
1'55"
Photo Credit
Tanzanian Peacekeepers/Kapteni Asia Hussein