Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

04 JANUARI 2023

04 JANUARI 2023

Pakua

Hii leo jaridani tunaangazia haki za wafungwa, na kazi za walinda amani nchini CAR.  Makala tutaelekea nchini Guatemala na mashinani leo tunarejea makao makuu ya umoja wa Mataifa ambapo utapata kauli ya Rais wa Baraza la Usalama kwa mwezi huu wa Januari kuhusu Syria.

  1. Kufuatia kuanza kwa maadhimisho ya miaka miaka 75 tangu kupitishwa kwa Tamko la Umoja wa Mataifa kuhusu haki za binadamu, UDHR, Kamishna Mkuu wa Umoja wa Mataifa wa haki za binadamu, Volker Türk ametoa wito kwa serikali duniani kote na mamlaka zote zinazoshikilia watuhumiwa kuwapatia msamaha au kuwaachilia huru wale wote walioswekwa ndani kwa kutekeleza haki zao za msingi.
  2. Mkuu wa Ujumbe wa Umoja wa Mataifa wa kulinda amani kulinda amani nchini Jamhuri ya Afrika ya Kati, CAR,  MINUSCA Kanda ya magharibi Brigedia Jenerali Zarrar Haider ametembelea kikosi cha 6 cha walinda amani wa Umoja wa Mataifa kutoka Tanzania, TANBAT 6 kilichoweka kambi Berberati, Mambéré-Kadéï.
  3. Makala tutaelekea nchini Guatemala kumwangazia mkimbizi ambaye sasa yuko mstari wa mbele kupambana dhidi ya mabadiliko ya tabianchi katika nchi iliyompokea, Guatemala.
  4. Na katika mashinani ambapo zimesalia siku 7 tu kabla ya kumalizika kwa muda wa azimio la makubaliano ya kufikisha misaada ya kibinadamu kati ya mpaka wa Uturuki na Syria. Akizungumza na waandishi wa habari mjini New York, Marekani Rais wa Baraza la Usalama mwezi huu Ishikane Kimihiro, mwakilishi wa kudumu wa Japan Umoja wa Mataifa ameahidi kulifanyia kazi azimio hilo. 

Mwenyeji wako ni Assumpta Massoi, karibu !

Audio Credit
Assumpta Massoi
Audio Duration
10'29"