Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

29 DESEMBA 2022

29 DESEMBA 2022

Pakua

Hii leo tunakuletea jarida maalum likimulika kwa muhtasari yaliyojiri mwaka huu na matarajio kwa mwaka 2023 na pia habari kwa ufupi zikiwemo heri ya mwaka mpya kutoka katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, hali ya usalama katika Greater Jonglei nchini Sudan Kusini na wanawake na wasichana kukatazwa kufanya kazi na mashirika yasiyo ya kiserikali NGOs. nchini Afghanistan.

  1. “Kila Mwaka Mpya ni wakati wa kuzaliwa upya”, ndivyo Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, Antonio Guterres alivyozianza salamu za mwaka mpya wa 2023 kwenda kwa ulimwengu.
  2. Shirika la Umoja wa Mataifa la kuratibu masuala ya kibinadamu na misaada ya dharura OCHA limesema takriban watu 30,000 wametawanywa kufuatia mapigano ya hivi karibuni ya watu wenye silaha kwenye eneo la greater Pibor.
  3. Na kamishina mkuu wa shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia wakimbizi UNHCR Filippo Grandi ameungana na wakuu wengine wa mashirika ya kibinadamu kutoa wito kwa serikali ya mpito ya Afghanistan kubadili maamuzi yake ya kuwazuia wanawake kufanya kazi na mashirika yasiyo ya kiserikali NGOs. 

Mwenyeji wako ni Anold Kayanda, karibu!

Audio Credit
Anold Kayanda
Sauti
13'58"