Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

21 DESEMBA 2022

21 DESEMBA 2022

Pakua

Hii leo jaridani tunamulika haki za wasichana na wanawake nchini Afghanistan na mkopo wa IMF nhini Kenya. Makala tunakupeleka nchini Zambia na mashinani tunakwenda nchini Mali kumulika UNICEF na harakati za kunasua watoto walioathirika na majanga yanayokumba taifa hilo.

  1. Umoja wa Mataifa umetaka mamlaka za watalibani nchini Afghanistani kubadili uamuzi wake wa kuzuia wasichana kujiunga na elimu ya Vyuo Vikuu nchini humo ambapo Katibu Mkuu wa Antonio Guterres amesema fursa ya elimu iwe kwa wote huku Mkuu wa haki za binadamu akisema hatua hiyo ni ukiukwaji mkubwa wa wajibu wa AFghanistan katika sheria za kimataifa za haki za binadamu. 
  2. Bodi tendaji ya Shirika la fedha duniani IMF imekamilisha awamu ya nne ya Ukaguzi wa Mpango wa Upanuzi wa Hazina kwa taifa la Kenya na kuipa nchi hiyo mkopo wa dola milioni 447.9li iweze kutekeleza mipango yake ya upanuzi na usaidizi wa mikopo.
  3. Makala tunaelekea kusini mwa Afrika hususan nchini Zambia kusikiliza changamoto zinazoweza kuhatarisha ustawi wa uvuvi katika ziwa Tanganyika kama si Mradi wa FISH4ACP unaoratibiwa na FAO kuhamasisha uvuvi endelevu..
  4. Na katika mashinani afisa wa shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia watoto UNICEF aanzungumzia kile wanachofanya Mali kusaidia watoto walioathiriwa na ukosefu wa usalama na mabadiliko ya tabianchi hadi kulazimika kukimbia makwao na sasa wanaishi kwenye kambi za wakimbizi ndani ya taifa hilo la Afrika Magharibi.

Mwenyeji wako ni Assumpta Massoi karibu!

Audio Credit
Assumpta Massoi
Audio Duration
12'7"