Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

20 DESEMBA 2022

20 DESEMBA 2022

Pakua

Hii leo jaridani tunakuletea mada kwa kina ambapo tunakupeleka nchini Tanzania kusikiliza simulizi ya raia wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, DRC ambaye baada ya kukimbia machafuko nchini mwake sasa ana hadhi ya uhamiaji nchini Tanzania. Pia tunakuletea habari kwa ufupi zikiwemo njaa Somalia, hatari za majanga, na madhara ya mazingira Iran. Mashinani tutaelekea nchini Msumbiji ambako tutashuhudia kuwa jamii ikiamua, hakuna mwanajamii atakayeachwa nyuma.

  1. Ingawa Umoja wa Mataifa ulitangaza kuwa baa la njaa limeweza kuepukwa kwa sasa nchini Somalia, Shirika la Umoja wa Mataifa la chakula na kilimo duniani, FAO limesema bado kuna muda wa kufanya mageuzi zaidi kuepusha kabisa baa la njaa  kwa kushughulikia mahitaji ya haraka ya jamii za vijijini ambazo ni miongoni mwa walio hatarini zaidi. 
  2. Mashirika ya Umoja wa Mataifa lile la Mpango wa maendeleo duniani, UNDP, Hali ya hewa Duniani WMO pamoja na ofisi ya Umoja wa Mataifa ya upunguzaji hatari za majanga UNDRR wanashirikiana kutengeneza mfumo mpya wa ufuatiliaji, kurekodi na kuchambua matukio ya hatari pamoja na hasara na uharibifu unaosababishwa na Matukio hayo.
  3. Wataalamu wa Umoja wa Mataifa wamesema kuwa vikwazo vilivyowekwa Marekani dhidi ya Iran ikiwemo kampuni za kigeni vina madhara kwa mazingira na vinazuia wananchi wa Iran, pamoja na wahamiaji na wakimbizi kutoka Afghanistan washindwe kufurahia kikamilifu haki zao za afya na maisha na wakati huo huo kusababisha madhara mengine kama vile uchafuzi wa hewa.
  4. Na mashinani tutakupeleka katika mji wa Chiure jimboni Cabo Delgado ambako Shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia watoto, UNICEF kwa kushirikiana na jamii pamoja na serikali wanafanikisha ndoto ya elimu kwa watoto kutoka hali mbalimbali za kimaisha kama mtoto Darwin mwenye umri wa miaka 9 pamoja na kuwa ni mwenye ulemavu, lakini miundombinu bora inasaidia. Jotas ni baba wa Darwin, anafurahi.

Mwenyeji wako ni Anold Kayanada, karibu!

Audio Credit
Anold Kayanda
Audio Duration
11'38"