Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

04 NOVEMBA 2022

04 NOVEMBA 2022

Pakua

Hii leo katika Habari za UN tunamulika haki za binadamu hasa za watu wenye ukoma, kisha teknolojia, wakimbizi na wahamiaji Rwanda na amani na usalama. kwa kina!

  1. Watu wenye ukoma na familia zao wamesubiri muda mrefu sana ili haki zao za kuwa na ulemavu ziweze kutambuliwa kitaifa na kimataifa, amesema mtaalamu huru wa Umoja wa Mataifa hii leo kwa ripoti yake kwa Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa.
  2. Janga la COVID 19 lilipotangazwa mwaka 2019 lilizua taharuki kila kona ya dunia lakini changamoto zilizoletwa na janga hilo zilikuwa fursa kwa vijana nchini Zimbabwe ambao walikuja na wazo la shule mtandaoni na Shirika la Umoja wa Mataifa la mpango wa maendeleo duniani, UNDP likawapatia fedha ili watekeleze wazo na kuwanufaisha wanafunzi wa shule za msingi na sekondari.
  3. Makala inatupeleka katika eneo la Nyarugenge mjini Kigali Rwanda ambako katika pitapita yake Flora Nducha wa Idhaa hii ya Kiswahili alipata fursa ya kuzungumza na baadhi ya mafundi cherahani wahamiaji kutoka Jamhuri ya Kimekrasia ya Congo DRC walioingia Rwanda kusaka mustakbali bora ikiwemo amani na usalama na kujitafutia riziki kwa sababu ya changamoto za usalama zinazoendelea nchini mwao.
  4. Mashinani tutasikia ujumbe Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa kuhusu ushiriki wa wanawake na vijana katika ujenzi wa amani na kuleta maendeleo.

Karibu na mwenyeji wako ni Assumpta Massoi

Audio Credit
ASSUMPTA MASSOI
Audio Duration
14'54"