Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

21 Machi 2022

21 Machi 2022

Pakua

Jaridani leo Machi 21, 2022 na Leah Mushi limeanza kwa habari kwa ufupi hususan-
Wanawake na wasichana wanaendelea kuishi maisha ya jehanamu nchini Sudan Kusini kutokana na unyanyasaji na ukatili ukiwemo wa kingono unaofanywa na makundi yote yenye silaha katika mzozo unaondelea nchini humo.
Misitu bora ni muhimu kwa ajili ya watu na sayari dunia amesema Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres katika ujumbe wake wa kuadhimisha siku ya kimataifa ya misitu hii leo.
Kongamano la 9 la maji duniani limefunguliwa leo mjini Dakar Senegal kwa shirika la Umoja wa Mataifa la elimu , sayansi na utamaduni UNESCO kwa niaba ya UN-Water kuzindua ripoti mpya ya Umoja wa Mataifa ya maendeleo ya maji duniani, iliyopewa jina "Maji ya chini ya ardhi: Kufanya visivyoonekana vionekane".

Katika mada kwa kina tunaangazia siku ya mashairi duniani, ambako tunamikia mshairi kutoka nchini Tanzania.

Audio Credit
Leah Mushi
Audio Duration
11'13"