Ushiriki wa viongozi wa dini katika kupambana na ukeketaji Tarime Tanzania waanza kuonesha mwanga
Ukeketaji unajumuisha taratibu zote zinazohusisha uondoaji wa sehemu au jumla yote ya sehemu ya siri ya nje ya mwanamke. Zoezi hilo mara nyingi hufanywa na waganga wa jadi na wanaokeketa wanajulikana kama mangariba. Ukeketaji unatambulika kimataifa kama ukiukaji wa haki za binadamu za wasichana na wanawake.
Umoja wa Mataifa umekuwa ukichagiza mbinu mbalimbali za kutokomeza vitendo hivi vya kikatili na nchi wanachama zimepokea wito huo na kutafuta namba tofautofauti za kupambana na hali hiyo ambayo imejikita katika utamaduni wa baadhi ya jamii ulimwenguni.