Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

UNHCR yatiwahofu na machafuko yanayoendelea Darfur

UNHCR yatiwahofu na machafuko yanayoendelea Darfur

Pakua

Machafuko yanayoendelea katika jimbo la Darfur nchini Sudan yamewasababisha maelfu ya watu kufungasha virago na kutyakimbia makazi yao tangu mwezi Novemba mwaka huu, wengi wakitawanywa ndani ya nchi na wengine kwenye mpaka wa nchi Jirani ya Chad limesema shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia wakimbizi UNHCR na kuongeza kluwa linatiwa hofu kubwa na hali hiyo.

Jason Nyakundi anasimulia zaidi 
Nattss…..  
Katika eneo la Darfur Magharibi video ya UNHCR ikidhihirisha hali halisi ya kilichotekea hapa , masalia ya nyumba zilizoteketezwa kwa moto na mahame.
Nattss......
Huyo ni mmoja wa wakazi  wa eneo hili Mustapha Mohamed akisema kundi la watu wenye silaha liliwavamia na halikuwaaliza lolote isipokuwa kuanza kuwahsmabulia na kuwafyatulia risasi. 

Kwa mujibu wa UNHCR karibu watu 10,000 wamekimbia mapigano haya mapya ya kijamii kwenye wilaya ya Jebel Moon jimbo la Darfur Magharibi na zaidi ya watu 2,000 miongoni mwao wakiwa ni wanawake na watoto ambao kwa sasa wanapata hifadhi katika maeneo ya jirani. 

Zacharia Mahmoud Adam ni mmoja wa watu hao waliotawanywa na machafuko haya anaeleza alichoshuhudia 
“Wamechoma moto kijiji chote, na tangu asubuhi tumefanikiwa kuwaokoa watu wanane tu waliojeruhiwa  na 9 waliouawa. Hivi sasa hatuna uhakika wa nini kinachoendelea kwa sababu barabara inayoelekea Krenik imefungwa na watu wameweka vizuizi barabarani.” 

Machafuko hayo, ukichanganya na msimu duni wa mvua na mlipuko wa wadudu kama nzige UNHCR inasema vimewaathiri kwa kiasi kikubwa wakulima Darfur huku wakulima waliotawanywa wakiliambia shirika hilo kwamba wanahofia kuambulia patupu wakati wa mavuno ukifika. 

Kutokana na ongezeko la hatari dhidi ya raia hivi sasa UNHCR inakutana na viongozi wa mamlaka ya maeneo husika kujadili hali ya inayoendelea na kuwahakikisha usalama rai lakini pia kuimarisha uratibu wa misaada ya kibinadamu ikiwemo ile inayohitajika haraka kama maji safi, chakula na malazi. 

Pia shirika hilo linakusanya msaada kwa ajili ya watu waliokimbilia nchi jirani ya Chad. Chad inahifadhi jum;a ya wakimbizi 520,000 na  asilimia 70 kati yao wanatoka Sudan. 

Audio Credit
Flora Nducha / Jason Nyakundi
Audio Duration
2'23"
Photo Credit
© UNICEF/Ron Haviv