Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Mafunzo yaliyotolewa na FAO Tanzania yawaongezea mavuno wakulima

Mafunzo yaliyotolewa na FAO Tanzania yawaongezea mavuno wakulima

Pakua

Kuelekea mkutano wa Umoja Mataifa kuhusu mifumo endelevu ya vyakula kuanzia shambani hadi mezani, huko mkoani Kigoma nchini Tanzania mradi wa pamoja Kigoma unaoendeshwa kwa pamoja na serikali na mashirika ya Umoja wa Mataifa likiwemo lile la chakula na kilimo, FAO umezidi kuwajengea kujiamini wakulima kwa kuwa hivi sasa kilimo chao kinahimili mabadiliko ya tabianchi na kiwango cha mavuno kimeongezeka bila uchovu ikilinganishwa na awali.
(Taarifa ya Anold Kayanda/Assumpta Massoi)

Ni Elizabeth Matanya huyu mkulima kiongozi kutoka Kibondo mkoani Kigoma na mnufaika wa mafunzo ya kilimo hifadhi cha mihogo, maharagwe na mahindi.
Eugene Hengama akiwa kwenye shamba lake la mahindi akafafanua walichofundishwa.

Kwa wakulima wa mihogo nao hawakuachwa nyuma kama asemavyo Japhet Magwala wa kikundi cha Tushirikiane.

Advera naye anaunga mkono akiongezea suala la faida ya kilimo na ufugaji.

Mafunzo ya FAO yamejengea uwezo wakulima kutambua udongo hai na hoi kama asemavyo Jackson Ntaziha akiwa na kifaa cha kupimia udongo.

Kwa mujibu Albert Fatakanwa ambaye ni afisa kiungo wa mradi wa KJP wilayani Kibondo, mradi umekuwa na manufaa siyo tu kwa wakulima bali pia halmashauri.

Audio Credit
Assumpta Massoi/Anold Kayanda
Audio Duration
4'8"
Photo Credit
FAO Tanzania