Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Changamoto zitokanazo na ugonjwa wa kisukari

Changamoto zitokanazo na ugonjwa wa kisukari

Pakua

Tukielekea siku ya kisukari duniani hapo kesho shirika la afya la Umoja wa Mataifa WHO linasema idadi ya wagonjwa wa kisukari duniani inaongezeka na ugonjwa huo unakatili maisha ya watu…. Kila mwaka. Ndio maana mwaka huu kaulimbiu ni waauguzi na kisukari ikiwa ni kampeni ya kuelimisha kuhusu umuhimu wa jukumu la watu hao katika vita dhidi ya kisukari.  Hata hivyo unapokuwa mkimbizi katika mkambini au makazi ya wakimbizi ukitegemea msaada kuweza kuishi kisukari ni msumari wa moto juu ya kidonda. Mwandishi wetu wa Uganda John Kibego amemtembelea mwanmke kutoka Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo (DRC), mmoja wa wakimbizi waanoishi na ugonjwa wa kisukari ili kufahamu changamoto anazopitia kuishi na ugonjwa huo hasa wakati huu wa COVID-19.
Je, kando na msaada kutoka mashirika ya kibinadamu yakiwemo ya Umoja wa Mataifa la chakula WFP na lile la afya WHO, anafanyaje kuona kwamba afya yake haizorori? Ungana naye katika mahojano yafuatayo.
 

Audio Credit
Flora Nducha/ John Kibego
Audio Duration
7'12"
Photo Credit
UN News/ John Kibego