Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Afrika kukumbana na changamoto ya malaria baada ya dawa maarufu ya artemisin kuwa sugu:Utafiti

Afrika kukumbana na changamoto ya malaria baada ya dawa maarufu ya artemisin kuwa sugu:Utafiti

Pakua

Watafiti wa malaria barani Afrika wameonya kuwa huenda bara hilo likajikuta katika hali ngumu ya kupambaan na ugonjwa wa malaria unaokatili maisha ya maelfu ya watu kila mwaka na hasa watoto wa chini ya umri wa miaka mitano. Hii ni baada ya wanasayansi nchini Rwanda kugundua kuwa vimelea vinavyosababisha ugonjwa wa malaria vimekuwa sugu kwa dawa maarufu na inayotumika sana kutibu ugonjwa huo ya Artemisin . Jason Nyakundi ameandaa ripoti hii.

Hii ndiyo mara ya kwanza wanasayansi wamegundua usugu kwa dawa hii barani Afrika.

Sasa watafiti wanaonya kuwa hii inaweza kuwa hatari kubwa kwa afya barani

Dr Mwaka Kakolwa ni mtafiti kutoka taasisi ya afya ya ifakara mjini Dar es salaam akifafanua  ni kwa nini ugonjwa wa malaria unageuka kuwa sugu."Wanasayansi kutoka taasisi moja ya utafiti nchini Ufaransa kwa ushirikiano na idara ya kupambana na ugonjwa wa malaria nchini Rwanda, shirikala afya duniani WHO, na chuo cha Columbia nchini Marekani walifanyia utafiti sampuli za damu kutoka kwa wagonjwa nchini Rwanda."

Waligundua kuwa mabadiliko fulani kwenye vimelea yalivifanya kuwa sugu kwa dawa ya kutibu malaria kwenye wagonjwa 19 kati ya 257 ya wagonjwa kwenye moja ya zahanati zilizokuwa chini ya uchunguzi.

Audio Credit
Assumpta Massoi\Jason Nyakundi
Audio Duration
2'4"
Photo Credit
Sven Torfinn/WHO 2016