Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Uganda yachukua hatua zaidi kuzuia kusambaa kwa COVID-19

Uganda yachukua hatua zaidi kuzuia kusambaa kwa COVID-19

Pakua

Serikali ya Uganda imeamua kufunga mipaka yake yote kwa abiria na kutangaza kuwa ni vyombo vyenye shehena za mizigo pekee ndio vitakavyovuka mipaka na kuingia nchini humo kufuatia kuthibitishwa kwa mgonjwa wa kwanza wa Corona au  coronavirus">COVID-19 nchini humo mwishoni mwa wiki. Maelezo zaidi na mwandishi wetu, John Kibego kutoka Kampala.
(Taarifa ya John Kibego)
Hatua hii imetangazwa katika hotuba ya Rasisi wa Uganda Yoweri Kaguta Museveni kwa taifa baada ya kisa cha kwanza cha virusi vya Corona aina ya COVID-19 kuthibitishwa humo ncjhini.
Kisa hicho kilithibitishwa usiku wa kuamkia tarehe 22 mwezi huu wa Machi na kutangazwa na Waziri wa Afya Dokta Jane Ruth Aceng kwenye mkutano wa wandishi wa habari.
Kisa hicho cha COVID-19 ni cha raia wa Uganda mwenye umri wa miaka 36 naliyekuwa amerejea nyumbani kutoka safari yake ya kibiashara mjini Dubai.
Kufuatia kisa hicho, huyu hapa Riais Museveni akibana usafiri wa aabiria, kuingia au kutoka ndani ya nchi.
(Sauti ya Museveni)
“Kutokana na utata wa kujaribu kudhibiti wasafiri kutoka nchi zilizoathiriwa sana, tuliamua kusitisha kabisa usafiri wa abiria kuingia au kutoka ndani ya Uganda. Ni bora tuokoe nyumbani ambayo ni Uganda na watu milioni 42 waliomo. Naam tunafahamu kuwa kuna Waganda nje ya nchi lakini kama tulivyokuwa tikufanya vitani ikiwa kambi imevamiwa, tunatoa kipaumbele kwa kushinda wavamizi wa kambi. Ndio maana tumesema hamna abiria tena iwe kwa ndege, nchi kavu au usafiri wa majini. Pia tumesema kwamba hatutakubali watu kuingia hata kwa basikeli au wanaotembea kwa mguu kupitia kwenye mipaka rasmi au isio rasmi kwani tutapeleka askari huko”
Kilithibitishwa saa chache baada ya ibaada maalum iliyofanyika kwneye ikulu ya Raisi ya Entebbe na kuhudhuriwa na karibu vyongozi wa dini zote kwa ajili ya kuliombea taifa lisisajili kisa chochote cha virusi hivyo na pia kumshukuru Mungu kwa kulilinda dhidi ya wmambukizo wakati ambapo nchi nne jirani za Tanzania, Rwanda, Kenya na Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC) zinakumbana na milipuko.
Mlipuko nchini Uganda pia umetangazwa siku tatu baada ya kufungwa kwa taasisi zote za elimu, masoko yanayolema na mikutano ya kisiasa na maeneo yote ya mijumwiko ya umma kama njia ya kuzuia mlipuko.
Magari, ndege na boti za mzigo ndizo zitakubaliwa kufanya kazi ya kuvuka mpaka lakini kwa masharti ya kuzingatia usadi na maagizo yote ya wizara ya afya na pia lazima kila chombo kimoja kisiwe na wafanyakazi wanaozidi watatu.
Raisi Museveni amewashauri wananchi wasitumie tena usafiri wa umma ikiwa wana uwezo wa kutumia usafiri binafsi au kujizuia safari sisizo za dharura.
Kwanzia jioni ya Ijumma, takribani watu 100 wamekamatwa na kuzuiliwa kwenye korokoroni mbalimbali kote nchini kuhusiana na kukaidi maagizo ya Raisi ya kinga dhidi ya COVID-19.

 

Audio Credit
Assumpta Massoi/ John Kibego
Audio Duration
2'42"
Photo Credit
UN Photo/Sarah Fretwell