Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

27 DESEMBA 2019

27 DESEMBA 2019

Pakua

Katika Jarida la mada kwa kina hii leo Flora Nducha anakuletea

-Wataalam wa haki za binadamu wa Umoja wa Mataifa wamelaani vikali hukumu ya kifo aliyopewa muhadhiri wa chuo kikuu cha Bahauddin Zakariya nchini Pakistan bwana Unaid Hafeez mwenye umri wa miaka 33  kwa madai ya kukashifu dini darasani na kwenye mtandao wa Facebook

-Mradi wa shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia wakimbizi UNHCR, shirika la Umoja wa Mataifa la uhamiaji IOM na serikali ya Brazili wa kuwahamisha wakimbizi wa Venezuela kutoka mashambani kwenda mijini umeleta matumaini mapya kwa wakimbizi hao

-Nchini Bangladesh kliniki mpya ya mazoezi ya viungo na kutibu maradhi kama ya kutetemeka na kukakamaa kwa wakimbizi wa Rohingya na jamii zinazowahifadhi imekuwa mkombozi wa maisha

-Mada yetu kwa kina hii leo inatupeleka katika chuo kikuu cha Nairobi nchini Kenya kumulika mafunzo ya lugha ya Kiswahili na jinsi lugha hiyo inavyopanua wigo

-Na katika kujifunza Kiswahili wiki hii tuko Baraza la Kiswahili la Kiswahili la Zanzibar , BAKIZA kufahamu maana ya methali "Mtaka cha uvunguni sharti ainame"

Audio Credit
UN News/Flora Nducha
Audio Duration
9'57"