Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Sheria ya kuwalinda wazee yatoa matumaini kwa wazee kukabiliana na madhila wanayoyapitia Tanzania

Sheria ya kuwalinda wazee yatoa matumaini kwa wazee kukabiliana na madhila wanayoyapitia Tanzania

Pakua

Nchini Tanzania kuna Sera ya wazee iliyotungwa mwaka 2003 lakini hadi sasa haijatungwa sheria ya kusimamia utekelezaji wa sera hiyo.Wazee wanasema kuwa sheria ya kuwalinda ndio muarobaoni wa changamoto za maisha wanazokabiliana nayo hasa kiuchumi kwani wanapoishiwa nguvu za uzalishaji, hukosa mahitaji ya msingi anayostahili binadamu. Katika kuendana na azma ya kutomuacha mtu yeyote nyuma ifikapo mwaka 2030, nchi nazo zinaweka sera, sheria na mikakati mbali mbali kuhakikisha hilo linatimia. Katika makala hii Tumaini Anatory wa radio washirika  Karagwe FM mkoani  Kagera nchini Tanzania amefuatilia suala hilo la hali ya wazee na matarajio ya kufuatia sheria hiyo, ungana naye.

Audio Credit
Brenda Mbaitsa/ Tumaini Anatory
Audio Duration
4'11"
Photo Credit
Picha ya UN