Kila mtoto ana haki ya fursa hata kama yuko tofauti-Lucy Gichana

10 Septemba 2019

Watoto wenye mahitaji maalum wanastahili haki sawa na wale wa kawaida hususan katika suala la elimu amesema Lucy Gichana mwanamke kutoka nchini Kenya ambaye kwa sasa anaishi Shangai nchini China akifundisha na kujitolea kwa watoto wenye mahitaji maalum wakiwemo wenye usonji. Akizungumza na Flora Nducha wa Idhaa ya Kiswahili katika makala hii Lucy amesema mara nyingi hususan katika nchi masikini watoto wenye mahitaji maalum hukosa fursa za kuonyesha vipaji vyao kutokana na changamoto mbalimbali ikiwemo vifaa, walimu na hata kuchanganywa na wale wenye hali ya kawaida wakati wao wanahitaji msaada zaidi suala ambalo amesema lilimhamasisha kufanya kazi na watoto wenye mahitaji maalum. Lakini je hicho ndio kilimfanya ajitolee pia? Ungana naye katika makala hii

Audio Credit:
Grace Kaneiya/ Flora Nducha/ Lucy Gichana
Audio Duration:
4'5"

 

♦ Tafadhali iwapo unataka kupokea taarifa kutoka UN News Kiswahili kila wakati zinapochapishwa jisajili  hapa.
♦ Pia unaweza kupakua apu ili kusikiliza matangazo yetu wakati wowote popote ulipo.
♦ Tembelea pia chaneli yetu ya Youtube na pia Soundcloud