Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Wanaotumia dini na imani kuleta mgawanyiko na mizozo wasipewe nafasi- Guterres

Wanaotumia dini na imani kuleta mgawanyiko na mizozo wasipewe nafasi- Guterres

Pakua

Kwa mara ya kwanza Umoja wa Mataifa inaadhimisha siku ya kimataifa ya kumbukizi ya waathirika wa ghasia zitokanazo na dini au imani ambapo Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres amesema ulimwengu unapaswa kupinga na kukataa wale ambao kwa mabavu na kwa uongo wanashawishi kujenga imani potofu, kuchochea mgawanyiko na kueneza hofu na chuki. Arnold Kayanda na maelezo zaidi.

Ujumbe wa Bwana Guterres katika siku hii inayoadhimishwa kwa mara ya kwanza leo Agosti 22, umeeleza kuwa, “kwa miezi michache iliyopita, tumeona ongezeko la idadi ya mashambulizi dhidi ya mtu mmojammoja na kulengwa kwa makundi kwasababu tu ya  dini au imani zao. Wayahudi wameuawa katika masinagogi, mawe katika makaburi yao yamechorwa alama ya za kibaguzi, waisalamu wamepigwa risasi misikitini, maeneo yao ya kidini yameharibiwa, wakristo wameuawa wakisali, makanisa yao yameteketezwa kwa moto.”

Bwana Guterres ameendelea kueleza kuwa mashambulizi mengi kama vile la New Zealand, Sri Lanka na Marekani, yamelenga mauhususi maeneo ya kuabudu. Na pia katika migogoro mingi kote duniani kutoka Syria hadi Jamhuri ya Afrika ya Kati, jamii nzima imeshambuliwa kwa kigezo cha imani yao.

“Dini zote kubwa zinahubiri uvumilivu na mshikamano wa amani katika hali ya utu. Tunatakiwa kupinga na kukataa wale ambao wale ambao kwa mabavu na kwa uongo wanashawishi kujenga imani potofu, kuchochea mgawanyiko na kueneza hofu na chuki. Kuna utajiri na nguvu katika utofauti. Siyo tishio” Amamesisisitiza Bwana Antonio Guterres.

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa amenukuliwa pia akiongeza kuwa, “hii leo tunashuhudia siku ya kwanza ya kimataifa ya kuadhimisha waathirika wa matendo ya vurugu yanayolenga dini na imani. Katika siku hiitunasisitiza msaada wetu kwa waathirika wa vurugu zinazotokana na dini na imani. Na tunaonesha msaada msaada huo kwa kufanya kila lililoko katika uwezo wetu kuzuia mashambulizi ya namna hiyo na kutaka wale wanaohusika kuwajibishwa.”

Bwana Guterres amehitimisha ujumbe wake kwa kutoa wito kwa dunia kuwa inatakiwa ili kusimama kutokomeza ubaguzi dhidi ya wayahudi, chuki dhidi ya uislam, kuteswa kwa wakristo na makundi mengine ya kidini, pamoja na aina zote za ubaguzi wa rangi,  ubaguzi wa utaifa, ukandamizaji na kuchochea vurugu, “sote tuna jukumu la kuheshimu tofauti zetu na kukukuza umoja wa amani.”

Audio Credit
Assumpta Massoi/Arnold Kayanda
Audio Duration
1'43"
Photo Credit
UN Photo/Rick Bajornas)