Tuishinde COVID-19 na tukomeshe chuki na ubaguzi:Guterres
Katika ujumbe wake wa siku ya kimataifa ya kuwaenzi waathirika wa ukatili kwa misingi ya dini na imani, ambayo kila mwaka huadhimishwa Agosti 22, Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres ameonya kuhusu ongezeko la ubaguzi wa rangi tangu kuzuka kwa janga la corona au COVID-19 kote duniani.