Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Wanawake nchini Kenya washika hatamu kusongesha amani

Wanawake nchini Kenya washika hatamu kusongesha amani

Pakua

Lengo namba 16 la malengo ya maendeleo endelevu, SDGs linataka uwepo wa amani na haki pamoja na taasisi thabiti za kusimamia masuala hayo. Pamoja na hivyo, lengo hilo linasisitiza ushiriki wa jamii nzima katika kutunza na kulinda amani, ikimaanisha pia wanawake ambao ndio waathirika wakubwa pindi amani inapotoweka. Ni kwa kuzingatia hilo sambamba na mazingira tatanishi yaliyotokea nchini Kenya baada ya  uchaguzi mkuu wa mwaka 2007, wanawake nao wameshika hatamu kusongesha amani. Miongoni mwao ni Millicent Otieno, mwanzilishi wa shirika lisilo la kiserikali LPCI , linalochagiza wanawake katika masuala ya amani na usalama nchini Kenya na Afrika mashariki. Akiwa jijini New York, Marekani hivi karibuni alihojiwa na Flora Nducha wa Idhaa ya Kiswahili ya Umoja wa Mataifa kuhusu harakati hizo ambapo hapa Millicent anaanza kwa kueleza wanachokifanya kuwajuisha na pia kuwahusisha wanawake katika masuala ya amani na usalama.

Audio Credit
Assumpta Massoi/Flora Nducha
Audio Duration
4'29"
Photo Credit
UNICEF/Samuel Leadismo