Skip to main content

Chuja:

ziwa albert

© UNICEF/Zahara Abdul

Mafuriko yavuruga ndoto za wanawake wa Ziwa Albert, Uganda

Mbali na janga la Janga la Corona au COVID-19 ambalo limeikumba dunia kwa zaidi ya miaka miwili, wananchi wa Uganda waishio karibu na Ziwa Albert kwa miaka hiyo miwili wamekuwa wakikabiliwa na changamoto ya ziada ya mafuriko.

Wanawake wanachama wa kikundi cha Kaizo Women’s Group (KWG) wilayani Hoima ni moja wapo ya vikundi ambayo mipango yao ilikwamishwa na atahri za mafuriko na ambao sasa wanaomba msaada wa kifedha kutoka serikali katika juhudi zao za kujikwamua kutokana na uharibifu wa maji huku wakikabiliana na janga la COVID-19.

Sauti
3'32"
UN/ John Kibego

Jamii ya Watyaba kandoni mwa Ziwa Albert nchini Uganda yatishiwa tena na mafuriko

Wakati mkutano wa Umoja wa Mataifa wa mabadiliko ya tabianchi COP26 unaendelea katika huko Glosgow na Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres akiwa amewaeleza viongozi wa ulimwengu kuwa ni muhimu kuchukua hatua sasa kwani wanadamu wanajichimbia kaburi, nchini Uganda jamii ya Watyaba, mojawapo ya jamii za walio wachache wanaoishi katika viunga vya Ziwa Albert, wanapaza sauti kwa serikali na shirIka  la Umoja wa Mataifa la kuhudumia wakimbizi, UNHCR kuwasaidia kutokana na madhara ya mabadiliko ya tabianchi.

Sauti
3'45"
UN/ John Kibego

Waganda wahaha kukabiliana na athari za mafuriko na COVID-19

Majanga asili yametishia juhudi za kufikia malengo ya maendeleo endelevu au SDGs katika nchi zote duniani. Uganda ni miongoni mwa nchi ambazo mwaka huu na mwaka jana 2020 zimeathiriwa moja kwa moja na mlipuko wa COVID-19 na kuongeza chumvi kwenye kidonda cha mafuriko makubwa kihistoria. 

Licha ya changamoto hizo, serikali inawatia moyo wananchi kufanya kazi kwa bidii na kwa busara ili kudhibiti madhara ya majanga haya hasa jamii za ziwani zinazikabiliwa zaidi na majanga hayo mawili wakati mmoja. Makala iliyoandaliwa na John Kibego ina maelezo zaidi.

Sauti
3'43"

02 Machi 2021

Hii leo jaridani, Flora Nducha anaanzia huko Somaliland ambako Umoja wa Mataifa umepeleka mashine za kuwezesha wagonjwa kuvuta hewa ya oksijeni wakati huu hospitali zimezidiwa kutokana na  janga la COVID-19 linaloleta mkwamo kwa wagonjwa kupumua. Kisha anammulika Mkurugenzi Mkuu mpya wa shirika la biashara duniani, WTO, Ngozi Okonjo-Iweala ambaye amenaza rasmi jukumu lake akiwa mwanamke wa kwanza na pia mwafrika wa kwanza kushika wadhifa huo.

Sauti
14'3"
UN/ John Kibego

Mabadiliko ya tabianchi yameacha kovu kwa wenyeji wa Ziwa Albert, Uganda.

Mafuriko makubwa ambayo yanayohusishwa na mabadiliko ya tabianchi, yameshuhudiwa katika meneo mengi duniani kote na yamekuwa yakiathiri watu kwa namna tofauti. Sudan, Sudan kusini, Uganda na India ni miongoni mwa nchi zilizoathirika na hali hii hususani katika kipindi cha kuelekea mwishoni mwa mwaka jana wa 2020. Ili kufuatilia maisha ya walioathirika na hali hii, mwandishi wetu wa Uganda John Kibego, amezungumza na Nyanjura Nyangoma mwanamke anayelea familia ya watoto 14 pembezoni mwa Ziwa Albert.

Sauti
3'49"
UNICEF/Tremeau

Msitu wa Bugoma ni uhai kwa maisha yetu-Uganda

Misitu ya asili kote duniani, kwa miaka mingi imekuwa sehemu muhimu ya maisha ya binadamu. Mathalani nchini Uganda, msitu wa Bugoma si tu unatunza historia ya asili ya watu wa eneo hilo, bali pia, wakazi wa eneo hilo wanasema vyanzo vingi vya maji ya mito ya eneo hilo ni katika mstu huo ambao pia unawapa dawa za asili za mitishamba zinazotumika katika tiba ya asili ya kiafrika. Katika makala ifuatayo, John Kibego, mwandishi wetu wa Uganda anapeperusha hewani maoni ya  wenyeji wa msitu wa Bugoma kuhusu tishio la kuchafuliwa kwa kiasi kukubwa cha msitu huo wa akiba.

Sauti
3'4"
UN/ John Kibego

Wanawake wachimba chumvi waomba msaada, walalamikia vikwazo vya kuzuia COVID-19, Uganda

Nchini Uganda,katika eneo la magharibi mwa nchi hiyo kandoni mwa ziwa Albert, wanawake wa eneo hilo wanaoegemea biashara ya uchimbaji na uuzaji chumvi maarufu kwa jina la chumvi ya Kibiro ambayo pamoja na matumizi ya kawaida ya mapishi hutumika pia katika dawa za asili wamejikuta katika wakati mgumu kwani ufikiaji wa maeneo ya ziwani umekubwa na changamoto lukuki ambazo ni pamoja na vikwazo vya usafiri vilivyowekwa na serikali ili kudhibiti kuenea kwa COVID-19, pia mafuriko yaliyoziba mtandao wa barabara, kufungwa kwa masoko, kufurushwa baadhi ya wakazi wa Ziwa Albert kwenye mialo iliobaini

Sauti
4'

17 Julai 2020

Leo Ijumaa ni mada kwa kina tunakwenda nchini Uganda ambako ingawa si msimu w amvua, Ziwa Albert linafurika kila uchao na kusababisha mamia ya watu kukimbia eneo hilo, huku wafanyabiashara wakipoteza mbinu zao za kujipatia kipato, COVID-19 ikiongeza chumvi kwenye kidonda cha makali ya maisha. Neno la wiki leo ni methali kutoka kwa mchambuzi wetu Aida Mutenyo nchini Uganda lakini kumbuka kuna muhtasari wa habari ukiangazia siku ya kimataifa ya Mandela kesho Jumamosi Julai 18. Mwenyeji wako ni Flora Nducha, karibu.

Sauti
9'58"