Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Takwimu zatumika zaidi hivi sasa Kenya kupanga maendeleo

Takwimu zatumika zaidi hivi sasa Kenya kupanga maendeleo

Pakua

Lengo la mkutano huu wa takwimu ni kutathmini na kujadiliana jinsi ya kuboresha idara za takwminu duniani kote ili kuhakikisha takwimu bora zinafikiwa ili kutimiza malengo ya maendeleo endelevu.

Hiyo ni kauli ya Collins Omondi mkurugenzi wa takwimu za uchumi kwenye ofisi ya taifa ya Takwimu nchini Kenya. Bwana Omondiakizungumza na Idhaa ya kiswahili kandoni mwa mkutano wa kila mwaka wa wakuu wa ofisi za takwimu za nchi wanachama wa Umoja wa Mataifa kwenye kikao cha 50 kinachokunja jamvi hii leo Makao Makuu ya Umoja wa Mataifa hapa mjini New York Marekani, amenielezea mabadiliko ambayo yamejitokeza katika sekta ya takwimu.

Audio Credit
Arnold Kayanda
Audio Duration
2'2"
Photo Credit
©FAO/Veejay Villafranca