Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Mabadiliko ya tabianchi yameathiri wote ikiwemo wafugaji- Bi Leina

Mabadiliko ya tabianchi yameathiri wote ikiwemo wafugaji- Bi Leina

Pakua

Jamii za wafugaji ni kundi ambalo namna ya kujipatia kipato inategemea mifugo na mifugo inatagemea lishe ambayo uwepo wake hivi sasa unakumbwa na madhara ya mabadiliko ya tabianchi. Madhara ya aina hiyo yamesababisha wanaharakati kujitokeza kuhakikisha kuwa ufugaji unaendelea na mifugo inapata malisho bora. Nchini Kenya Agnes Leina ambaye ni mwanzilishi wa shirika lisililo la kiserikali la Illaramatak Community Concerns linalenga jamii za wafugaji. Kwa mujibu wa Bi. Leina, mabadiliko ya tabianchi yameathiri jamii hizo kwani kunashuhudiwa vipindi virefu vya kiangazi na sasa wamechukua hatua. Basi ni nini wanafanya ili kusaidia wenyeji ungana na Grace Kaneiya katika Makala ifuatayo.

 

Soundcloud
Audio Credit
Arnold Kayanda/ Grace Kaneiya/ Agnes Leina
Audio Duration
3'25"
Photo Credit
UNAMID/Albert González Farran