Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Vikosi vya Umoja wa Mataifa Sudan Kusini vinawapeleka wanafunzi shuleni na kuwarudisha nyumbani wakati wa mitihani.

Vikosi vya Umoja wa Mataifa Sudan Kusini vinawapeleka wanafunzi shuleni na kuwarudisha nyumbani wakati wa mitihani.

Pakua

Walinda amani Sudan Kusini wasindikiza wanafunzi shuleni na kuwarudisha nyumbani wakati wa mitihani.Polisi waliopo kwenye ujumbe wa Umoja wa Mataifa nchini Sudan Kusini  wamepewa jukumu la kuwasindikiza wanafunzi hadi kwenye kituo cha mtihani kwenye mji mkuu wa Sudan Kusini, Juba.  Usindikizaji huo unafanyika Kwa wiki mbili ambapo askari hao wataendelea kuwapeleka na kuwarudisha wanafunzi kufanya mitihani yao kwa usalama.

Bado ni alfajiri na kuna giza lakini polisi wa Umoja wa Mataifa nchini Sudan Kusini wameshafika katika eneo la kukutania tayari kupata maelekezo ya siku.

Elizabeth Peter mwanafunzi mwenye umri wa miaka 32 anajisomea kwa dakika za mwisho kabla ya kuelekea kwenye chumba cha mitihani.

“Mafanikio yangu yatawahamasisha watoto kwasababu watoto wanatakiwa kwenda shule maana elimu ni mstakabali wa watoto na nchi”

Ujumbe wa Umoja wa Mataifa nchini Sudan Kusini UNMISS unasema ili safari iwe salama ni lazima kuwepo mipango ya kina, mathalani Afisa wa polisi na mwalimu wanatakiwa kuwa katika kila basi,  njia ya kupita inapangwa na ulinzi unawekwa njiani na katika kipindi chote cha kufanya mtihani na eneo la shule.

Sarah Kerr,mmoja wa wanafunzi wanaofanya mitihani anasema, “tunajisikia fahari kwamba usalama umetuzunguka. Wametuleta hapa. Wanatutendea vizuri. Wanahakikisha mazingira ambayo tunafanyia mitihani yanafaa na salama. Ndiyo, hiyo ni safi, ninajikia furaha”

Baadhi  ya wanafunzi hawa ambao ni miongoni mwa wanaoishi katika vituo vya ulinzi wa raia tangu mwaka 2013 wakati mgogoro ulipoanza nchini Sudan Kusini wana ndoto za kuwa wanashera na viongozi na matumaini yao ni kuwa wataweza kuhakikisha kunakuwepo na amani ya kudumu na uatawala wa sharia katika nchi ambayo imeathirika na miaka mingi ya migogoro na mifumo iliyoharibika.

Audio Credit
Ramadhani Kibuga
Audio Duration
1'57"
Photo Credit
Picha na UNMISS