Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

15 Oktoba 2018

15 Oktoba 2018

Pakua

Jaridani leo Anold Kayanda anaanzia huko Roma Italia ambako kumezinduliwa ripoti mpya kuhusu chakula na kilimo ambapo uhamiaji wa ndani umepatiwa kipaumbele zaidi. Anabisha hodi Tanzania ambako Shirika la chakula na kilimo FAO nchini humo limetaja siri ya Tanzania kufanikiwa kwenye uhakika wa chakula.  Anakwenda Mashariki ya Kati ambako mtoto aitwaye Asmaa analalama kuhusu mazingira ya shuleni kwao. Makala  leo ni Vietnam kilimo kinachojali mazingira chaleta nuru kwa wakulima wa chai ilhali mashinani nako tunaelekea Kenya. Karibu!

Audio Credit
Arnold Kayanda
Audio Duration
10'44"