Kazi yetu ni muhimu lakini mara nyingi haijulikani- Mfasiri
Pakua
Tafsiri kutoka lugha moja hadi nyingine imekuwa ina mchango mkubwa katika utekelezaji wa majukumu ya Umoja wa Mataifa, amesema Lydie Mpambara, mmoja wa wafasiri wa lugha kwenye idara ya Baraza Kuu na mikutano ya Umoja huo, DGACM.
Akihojiwa na Idhaa ya Kiswahili ikiwa sehemu ya maadhimisho ya siku ya tafsiri ya lugha duniani iliyoadhimishwa hivi karibuni, Bi. Mpambara ambaye anazungumza kiingereza, kifaransa, Kiswahili na kispanyola amefafanua jinsi kazi yao inavyochagiza majukumu ya Umoja wa Mataifa.
Audio Credit
Siraj Kalyango
Sauti
2'23"