Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

FAO Tanzania na harakati za kuinua wakulima mkoani Kigoma

FAO Tanzania na harakati za kuinua wakulima mkoani Kigoma

Pakua

Nchini Tanzania, Umoja wa Mataifa kupitia mashirika yake unatekeleza mpango wa pamoja wa kuchagiza maendeleo mkoani Kigoma ukiwa unalenga maeneo kadhaa. Maeneo hayo ni pamoja na kilimo ambamo kwacho wakulima wanapatiwa mbinu za kilimo kinachohimili mabadiliko ya tabia nchi lakini pia kilimo na ufugaji unaoimarisha lishe kwa kaya. Ni kwa kuzingatia hilo shirika la chakula na kilimo duniani FAO nchini humo hivi karibuni limeendesha mafunzo kwa wakulima wakufunzi ili nao pia waweze kufundisha wakulima wenzao na hatimaye kilimo kishamiri, lishe iwe bora na kipato cha kaya kiongezeke, bila kusahau kutunza na kuhifadhi mazingira, yote hayo miongoni mwa malengo ya maendeleo endelevu, SDGs. Je wanufaika wanasema nini? Assumpta Massoi kwa msaada wa FAO  Tanzania amezungumza na baadh iya wanufaika na mmoja wao anaanza kwa kujitambulisha.

 

Audio Credit
Assumpta Massoi
Audio Duration
4'7"
Photo Credit
FAO/Olivier Asselin