Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

21 Agosti 2018

21 Agosti 2018

Pakua

Katika jarida maalum hii leo sikukuu ya Eid El Haj Assumpta Massoi anamulika wahudumu wa kibinadamu ambao kutwa kucha wanaweka rehani maisha yao ili kusaidia wale walio na mahitaji zaidi kuanzia Afrika, Asia, Ulaya, Pasifiki hadi Amerika, Jarida hili maalum linazingatia kuwa katika siku ya kimataifa mwaka huu ya usaidizi wa kibinadamu, kipaumbele kilielekezwa kwa watoa huduma za kibinadamu. Jarida linajikita Uganda lakini pia tutawajumuisha mashabiki wetu juu ya maoni yao kuhusu kifo ya Katibu Mkuu wa 7 wa Umoja wa Mataifa Kofi Annan. Annan alikuwa mwafrika wa kwanza mweusi kushika wadhifa huo. Kama ujuavyo kabla yake alikuwepo Boutros Boutros-Ghali kutoka Misri. KARIBU!

Audio Credit
Assumpta Massoi/John Kibego/Grace Kaneiya
Audio Duration
9'56"