Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Kampeni ya kupinga utoro shuleni na utumikishwaji wa watoto yazinduliwa Tanzania

Kampeni ya kupinga utoro shuleni na utumikishwaji wa watoto yazinduliwa Tanzania

Pakua

Utoro mashuleni ni moja ya tishio kubwa la kutotimiza lengo namba nne la maendeleo endelevu lihusulo elimu kama hautodhibitiwa nchini Tanzania. Sasa serikali imeamua kulivalia njuga suala hilo kwa kampeni ya mkoa kwa mkoa na mkono wa sheria.

Kampeni hizo ni za kuihamasisha jamii kuelewa umuhimu wa elimu, kuwafikisha mahakamani wazazi wasiohimiza watoto kwenda shule au wanaowafanyika kazi watoto badala ya kuwapeleka shule , lakini pia maandamano ya amani kama yaliyofanyika mkoani Tabora wiki hii na kuhususisha viongozi wa serikali, waalimu, wazazi na wahusika wakuu ambao ni wanafunzi.

 

Audio Credit
Patrick Newman
Audio Duration
3'28"
Photo Credit
Wanafunzi wa shule ya sekondari ya wasichana ya Weruweru nchini Tanzaniwa wakiwa wamebeba mabango ya malengo ya maendeleo endelevu, SDGs kutoka namba 1 hadi 5. (Picha: UNRCO/Mariam Simba)