Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Mvua iko njiani, inakuja turudi nyumbani kulinda mifugo yetu

Mvua iko njiani, inakuja turudi nyumbani kulinda mifugo yetu

Pakua

Tatizo la tabianchi ni suala mtambuka, ambalo Umoja wa Mataifa na washirika wake  wamekuwa wakilivalia njuga kuhamasisha serikali mbalimbali na asasi za kiraia  kuhusu ushiriki wa kila mtu katika ulinzi wa mazingira.

Mpaka sasa, ni wazi kwamba madhara ya uharibifu  wa mazingira yameshaanza kuonekana kila kona ya dunia.  Baadhi ya nchi katika bara la Afrika zinakabiliwa na tatizo la ukame, hivyo kusababisha jamii za vijijini kuathirika zaidi kwa ukosefu wa mvua, mazao kukauka, maji na huduma  zingine za msingi.

Kwa muktadha huo shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia watoto, UNICEF katika kampeni mbalimbali za kusaidia jamii za vijijini wamekuwa  wakiwatumia  watu maarufu kuhamasisha  jamii kupitia nyimbo, sanaa na maonyesho. Miongoni mwao ni msanii Kennedy Ombima, al maaruf kama King Kaka akimshirikisha Ayub Ongada kwenye kampeni hiyo ya UNICEF kuhusu ukame huko Turkana nchini Kenya. Nini kinajiri kwenye wimbo huo? Patrick Newman  anakuletea kwa kina burudani hiyo yenye mafunzo

Audio Credit
Siraj Kalyango/ Patrick Newman
Audio Duration
4'40"
Photo Credit
FAO/Simon Maina