Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Hii ni dunia moja hakuna haja ya kuiharibu-Guterres

Hii ni dunia moja hakuna haja ya kuiharibu-Guterres

Sisi binadamu hatuna ruhsa  kuangamiza hii dunia moja, ama kukubali tofauti zetu kusababisa mateso na maumivu ambavyo vinatuzuia kufaidika na manufaa ya ustaarabu.
Hayo ni maneno ya Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, Antonio Guteress, akihutubia wandishi habari mjini Backara Sweden bada ya kuwasili huko ambako yeyé na baraza la usalama watakuwa na kikao maalum  cha faragha huko katika nyumba ya katibu mkuu wa zamani  wa Umoja wa Mataifa  Dag Hammarskjöld.
(SAUTI YA GUTERESS)
‘’Na ninaposhuhudia yanayoendelea leo , tunapoona migawanyiko mingi, migawanyiko ya zamani ikirejea, migawanyiko mipya ikiongezeka mara dufu, migogoro ambayo inasababisha mateso makubwa duniani kote, na Syria ikiwa ndio mfano wa yote, ni muhimu kukumbuka maneno ya Dag Hammarskjöld.’’

Ameongeza kuwa Dag Hammarskjöld leo anabaki kama nembo madhubuti na mfano wake ni muhimu kwao kuweza kufanya mambo ambayo ni sawa, ilikuweza kuepuka utata na tofauti pamoja na kuelewa kwamba sote ni sharti tufanye kila liwezekanalo kuwa na dunia moja.
Pia Katibu Mkuu amegusia Korea Kaskazini kuhusu uamuzi wake kusimamisha kwa muda majaribio yake ya nuklia pamoja na urushaji wa  makombora yake ya masafa marefu.
(SAUTI YA GUTERESS)
“ Ninaiamini Korea kaskazini, mlango baado uko wazi na   azma vya kusaidia kwa njia za  amani  kuondoa silaha za nuklia kutoka rasi ya Korea.”
Pia amekariri azma ya uungwaji mkono wa mfumo wa Umoja wa Mataifa kutanzua mgogoro huo tena kwa njia za amani.

Pakua
Audio Credit
Flora Nducha
Audio Duration
1'55"
Photo Credit
Picha na Moa Haeggblom