Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Michezo kwa amani na maendeleo

Michezo kwa amani na maendeleo

Pakua

Shirika la Umoja wa Mataifa la wakimbizi UNHCR leo Ijumaa limezindua rasmi ziara itakayofika kila kona ya dunia kuonyesha mshikano na wakimbizi. Siraj Kalyango na ripoti kamili.

(Taarifa ya Siraj Kalyango)

Shirika hilo linasema lengo kuu la ziara hiyo ni kuelimisha na kuchagiza umma kuchukua hatua kwa ajili ya watu waliolazimika kukimbia mizozo au mateso.

Ziara hiyo ikipatiwa jina la kampeni ya kimtandao Hashtagwithrefugees inaanzia kwenye kambi ya wakimbizi ya Za'atari nchini Jordan inayoahifadhi wakimbizi 79,000 kutoka syria, ikiambatana na michezo mbalimbali kwa ajili ya maadhimisho ya siku ya kimataifa ya michezo kwa ajili ya amani na maendeleo.

Kwa mujibu wa mkuu wa kampeni, Leigh Foster, matukio hayo na mabalozi wema wa UNHCR, kuchukua hatua kutawafanya watu kuonyesha mshikamano na kujali kwao kuhusu wakimbizi kwani kila hatua inayochukuliwa ni muhimu.

 Matukio mengine yaliyopangwa katika ziara hiyo ya kimataifa ni pamoja na maonyesho ya mavazi yatakayofanyika Chicago yakijumuisha mavazi yatokanayo na vitambaa vilivyotengenezwa na wakimbizi nchi Kenya, mechi ya wakimbizi ya mpira wa miguu nchini Ireland, maonyesho ya picha mjini Paris, juma zima la matukio mbalimbali ya uelimishaji kisiwani Jeju korea Kusini na mashindano ya judo na tamasha nchini Afrika Kusini.

 Na ziara itafunga pazia Oktoba Mosi kwenye sherehe za tuzo ya wakimbizi ya Nansen inayotolewa na UNHCR mjini Geneva Uswisi.

Audio Credit
Siraj Kalyango
Audio Duration
1'28"
Photo Credit
UN/ Tobin Jones