Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Kelele za ubaguzi zikizidi uwanjani, tokeni

Kelele za ubaguzi zikizidi uwanjani, tokeni

Wachezaji mpira wanapokumbwana kauli za kibaguzi kutoka kwa mashabiki uwanjani, wachukue hatua ikiwemo kutoka uwanjani, amesema Kamishna Mkuu wa haki za binadamu Zeid Ra’ad Al Hussein.

Akizungumza na waandishi wa habari hii leo huko Geneva, Uswisi Bwana Zeid amenukuu mazungumzo yake na mwanasoka wa kulipwa nchini Ujerumani mwenye asili ya Afrika Kevin Prince Boateng, aliyemweleza kuwa ubaguzi viwanjani bado umeshamiri.

(Sauti ya Zeid Ra’ad Al Hussein)

“Wanacheza mchezo unaohusisha kupiga yaani kupiga mpira, sasa katika hali hiyo wao wenyewe wanaweza kujikuta wakipigwa au kushambuliwa na mashabiki na iwapo makamisaa wa mchezo hawafanyi lolote dhidi ya hilo basi  mtu anatumai kuwa wachezaji wenyewe wanaweza kujisimamia, wakaungana na kuchukua hatua na hata kutoka  uwanjani.”

Kamishna Zeid amesema wachezaji wengi wana wafuasi lukuki kwa hivyo kwa kuchukua hatua hiyo wanaweza kubadili mtazamo na fikra za kibaguzi dhidi ya wachezaji wa Afrika au wenye asili ya Afrika.

 

Pakua
Audio Credit
Assumpta Massoi
Audio Duration
1'3"
Photo Credit
UNHCR/Linh Dang