Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

WHO yatoa mwongozo dhidi ya mafua makali

WHO yatoa mwongozo dhidi ya mafua makali

Pakua

Msimu wa mafua makali tayari umebidha hodi katika nchi kadhaa huku ukinyemelea mataifa mengine, limesema shirika la afya duniani, WHO.

Kutokana na hali hiyo WHO imetoa mwongozo wa kuzingatia wakati wa msimu huu wa mafua makali ambapo baadhi ya nchi zimepata idadi kubwa zaidi ya wagonjwa.

Nchini Marekani viwango vya wanaokwenda hospitalini kutibiwa mafua  ni sawa na  vile vilivyotokea misimu saba iliyopita.

Maeneo ya tropiki kama vile barani Afrika, taarifa za visa vya mafua zimeripotiwa katika nchi kama vile Madagascar, ilhali  bara la Asia nchi za Pakistan na Singapore ndiyo zinaongoza.

Kwa mantiki hiyo WHO imependekeza nchi ambazo tayari zinakabiliwa na ugonjwa huo kupatia chanjo makundi ambayo yanakabiliwa zaidi na mafua hayo.

WHO inasema njia bora ya kuzuia mafua hayo ni chanjo ambapo hutolewa kabla ya kuanza kwa msimu wa ugonjwa huo na inashauriwa mtu apatiwe chanjo kila mwaka kwa sababu kila mara virusi vya mafua hubadilika.

 

Audio Credit
Siraj Kalyango
Audio Duration
1'4"
Photo Credit
UN/maktaba