Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Vijana ni ufunguo wa SDGs- Masalu

Vijana ni ufunguo wa SDGs- Masalu

Pakua

Vijana wana mchango mkubwa katika kusongesha ajenda ya mwaka 2030 ya maendeleo endelevu au SDGs . Hayo yamesisitizwa katika jukwaa la vijana la Umoja wa Mataifa 2018 lililokunja jamvi hii leo kwenye makao makuu ya Umoja huo New York Marekani. Vijana 700 kutoka nchi mbalimbali wamejadili jinsi gani washirikishwe na mchango wao katika kufanikisha azma hiyo ya Dunia. Miongoni mwa waliohudhuria ni kijana Paschal Masalu kutoka nchini Tanzania ambaye ni afisa mtendaji wa jukwaa la Elimikawikiendi nchini humo. Amezungumza na Flora Nducha wa idhaa hii kuhusu yaliyojiri katika jukwaa hilo na hasa yapi aliyokuja kuyawasilisha kwenye jukwaa hili kutoka wa vijana wa kitanzania

Audio Credit
Mahojiano ya Flora Nducha na Paschal Masalu
Audio Duration
3'43"