Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

UM waenzi waathirika wa mauaji ya Srebrenica

UM waenzi waathirika wa mauaji ya Srebrenica

Pakua

Umoja wa Mataifa leo Jumanne umewakumbuka na kuwaenzi maelfu ya wanaume na wavulana waliouawa kinyama miaka 22 iliyopita kwenye mji wa Srebrenica huko Bosnia na Herzegovina wakati wa vita vya Balkan.

Mauaji ya halaiki ya Julai 11 mwaka 1995 yalikuwa ndio makubwa zaidi kutokea katika ardhi ya jumuiya ya Ulaya tangu jumuiya hiyo ilipoanzishwa baada ya vita vya pili vya dunia. Katika taarifa yake Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa António Guterres amesema jumuiya ya kimataifa na hasa Umoja wa Mataifa wamekubali kubeba sehemu ya jukumu lao kuhusu zahma ya Srebrenica na wamejitahidi kujifunza kutokana na makosa.

Ameeleza kwamba kibarua kigumu cha kujenga upya imani ili kuruhusu maridhiano Bosnia na Herzegovina kipo mikononi mwa watu wa jamii mbalimbali za taifa hilo na kuongeza kwamba ili kujenga jamii bora na mustakhbali wa pamoja , majanga yaliyopita ni lazima yatambuliwe na jamii hizo.

Photo Credit
Ni mwaka 1995 mwanajeshi wa kitaifa akisoma orodha ya majina ya wanajeshi waliokimbia au manusura wa mji uliosambaratika wa SrebrenicaUNICEF/NYHQ1995-0553/LeMoyne