Baraza la haki za binadamu lakaribisha maridhiano Sri Lanka kwa tahadhari

Baraza la haki za binadamu lakaribisha maridhiano Sri Lanka kwa tahadhari

Pakua

Maridhiano nchini Sri Lanka baada ya miongo ya vita vya wenye kwa wenyewe yanafanyika sasa , lakini bado kuna kazi kubwa ya kufanya ili kuwafikisha kwenye mkono wa sheria waliokiuka haki za binadamu , amesema leo kanishina mkuu wa haki za binadamu wa Umoja wa mataifa Zeid Ra’ad Al Hussein.

Akizungumza kwenye baraza la haki za binadamu mjini Geneva, Bwana Zeid amekaribisha mabadiliko ya serikali kuhusu masuala yanayojumuisha udhibiti mkubwa katika jeshi.

Lakini Kamishina Mkuu ameelezea wasiwasi wake kwamba serikali Colombo haijachapuka kujenga mikakati ya imani miongoni mwa watu na hususani wahanga wa vita.

Zeid pia amesema ingawa ni zaidi ya miaka 25 tangu vita hivyo baina ya serikali na waasi wa Tamil Tigers vilivyokwisha 2009, utamaduni wa kufuatilia watu na kuwatisha bado unaendelea.

Photo Credit
Kikao cha Baraza la Haki za Binadamu. Picha: Umoja wa Mataifa/ Jean-Marc Ferré