Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Hukumu ya Radovan Karadzic ni hatua muhimu: Zeid

Hukumu ya Radovan Karadzic ni hatua muhimu: Zeid

Pakua

Kamishina mkuu wa Umoja wa mataifa wa haki za binadamu Zeid Ra’ad Al Hussein amekaribisha hukumu dhidi ya Radovan Karadzic, aliyekuwa Rais wa zamani jamhuri ya Serbina ya Bosnia Hergzegovina , iliyotolewa leo na mahakama ya kimataifa ya uhalifu kwa ajili ya Yugoslavia ya zamani ICTY, akieleza kwamba hukumu hiyo ni hatua muhimu sana.

Karadzic amekutwa na hatua ya mauaji ya kimbari, uhalifu dhidi ya binadamu na uhalifu wa vita. Zeid ameongeza kuwa miaka 21 baada ya kushitakiwa Karadzic hukumu hii ni dhihirisho la dhamira ya jumuiya ya kimataifa kutolifumbia macho suala la uwajibikaji. na amehukumiwa kwenda jela miaka 40. Hivi ndivyo hukumu yake ilivyotolewa

(SAUTI YA MWENDESHA MASHITAKA)

Karadzic alipanga kufungwa, kubakwa, kuteswa na kuuawa kwa maelfu ya watu , kushambuliwa kwa raia, kuzingirwa kwa Sarajevo;uharibifu wa hali ya juu na kubomolewa kwa maeneo ya kuabudu yakiwemo ya Waislamu na wakatoliki.

Zeid ameongeza kuwa hukumu yake ni ishara yenye nguvu sana hasa kwa waathirika na uhalifu uliotekelezwa wakati wa vita vya Bosnia-Herzegovina na Yugoslavia ya zamani , lakini pia kwa waathirika kote duniani.

Amesema licha ushawishi mkubwa walionao, haijalishi wanavyojihisi kwamba hawawezi kuguswa na haijalishi wanatoka bara gani, waliotekeleza uhalifu huo ni lazima watambue kwamba asilani hawatokwepa sheria

Photo Credit
Radovan Karadzic, aliyekuwa Rais wa zamani jamhuri ya Serbia ya Bosnia Hergzegovina.(Picha:ICTY)