Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Ban na salamu kuelekea mwaka mpya wa China wenye ishara ya tumbili

Ban na salamu kuelekea mwaka mpya wa China wenye ishara ya tumbili

Pakua

Leo tarehe nane Februari ikiwa ni maadhimisho ya mwaka mpya wa kichina 2016 na ukiwa na ishara ya tumbili mwekundu, Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-moon ametuma ujumbe wake akitaka jamii kuzingatia sifa za mnyama huyo katika maisha ya kila siku.

Ban amesema wanajimu wa kichina wanatambua kuwa mwaka 2016 ni mwaka wa moto na hivyo mwaka wa moto na tumbili mwekundu unamaanisha shauku, furaha na ubunifu.

Amenukuu usemi wa nchi atokayo Korea Kusini ya kwamba hata tumbili huanguka kutoka mtini, ikimaanisha kuwa kila mtu anaweza kufanya makossa.

Hata hivyo licha ya tumbili kuanguka mtini hapotezi kasi na wepesi wake kwani hunyanyuka na kuendelea na safari, hivyo kila mtu anapaswa kunyanyuka na kupanda hadi kufikia anga.

Photo Credit
kima punju msitu wa Jozani, Zanzibar (Picha ya Idhaa ya Kiswahili/Priscilla Lecomte