Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Dansi yatumika kupinga ajira kwa watoto

Dansi yatumika kupinga ajira kwa watoto

Pakua

Kutokomeza ajira kwa watoto ni jambo linalopigiwa chepuo kila uchao kutokana na kitendo hicho kutishia mustakhbali wao. Watoto wanapoajiriwa, haki zao kuu nne za msingi zinakuwa mashakani. Mathalani kiafya wanakuwa hatarini kupata magonjwa kutokana na kutumikishwa kwenye mazingira hatarishi, kielimu hawana muda wa kwenda shule. Hata hivyo Kampeni za shirika la kazi duniani ILO ikiwemo ile ya kadi nyekundu kwa wanaoajiri watoto inazaa matunda. Mathalani mwaka 2000 duniani kote kulikuwepo na watoto Milioni 240 wanaotumikishwa lakini sasa idadi imepungua hadi Milioni 168. Na bado kampeni inaendelea kama anavyotanabaisha Assumpta Massoi kwenye Makala hii.

Photo Credit
Wakati wa dansi.(Picha ya ILO/Video capture)