Harakati za kupambana na Malaria na changamoto zinazoibuka Mwanza Tanzania
Wakati dunia inaelekea kuadhimisha siku ya Malaria duniani tarehe 25 mwezi huu, ripoti za shirika la afya duniani, WHO zinasema kuwa kiwango cha vifo vitokanavyo na Malaria duniani kimepungua kwa asilimia 48 kwa watoto wenye umri wa chini ya miaka mitano kuanzia mwaka 2000 hadi 2012.