Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

UN: Watoto zaidi ya 560,000 wamepata chango ya polio katika duru ya kwanza ya kampeni ya chanjo Gaza

UN: Watoto zaidi ya 560,000 wamepata chango ya polio katika duru ya kwanza ya kampeni ya chanjo Gaza

Pakua

Zaidi ya watoto 560,000 wamepokea chanjo dhidi ya virusi vya polio aina ya pili (cVDPV2) kwenye Ukanda wa Gaza katika duru ya kwanza ya kampeni kubwa ya chanjo iliyomalizima jana yamesema mashirika ya Umoja wa Mataifa.

Kwa mujibu wa taarifa ya Shirika la Afya la Umoja wa Mataifa Duniani WHO, watoto waliopokea chanjo hiyo kupitia kampeni ya dharura ya chanjo Gaza ni wale wenye umri wa chini ya miaka 10.

Kupitia ukurasa  wake wa mtandao wa X zamani Twitter Mkurugenzi Mkuu wa WHO, Dkt. Adhanon Ghebreyesus amesema “Tunafurahia timu zote za wahudumu wa afya, zilizoendesha operesheni hii ngumu. Tunashukuru sana kwa familia kwa imani na ushirikiano wao. Haya ni mafanikio makubwa huku kukiwa na hali mbaya ya kila siku ya maisha katika Ukanda wa Gaza. Hebu fikiria nini kingeweza kufikiwa endapo kungekuwa na ushitishwaji mapigano.”

Awamu ya kwanza ya chango ilianza Septemba Mosi na lengo lilikuwa ni katika kila duru kuchanja  zaidi ya watoto 640 000 wa umri wa chini ya miaka 10.

Nalo shirika la Umoja wa Mataifa la msaada kwa wakimbizi wa Kipalestina UNRWA limesema maelfu kwa maelfu ya watoto wmechanjwa na kukamilika kwa awamu hiyo ya kwanza ya chanjo ni mafanikio makubwa kwa shirika hilo na wadau wote walioshiriki kwani wamefikia lengo kwa asilimia 90 ingawa sasa changamoto ni kutoa dozi ya pili ya chanjo hiyo katika awamu ya pili ya kampeni inayotarajiwa katika wiki zijazo.

Dozi za chanjo ya polio zaidi ya milioni 1.6 ziliwasili Gaza ili kukamilisha awamu zote mbili za chanjo inayohusisha wahudumu wa afya zaidi ya 2700.

Audio Credit
Cecily Kariuku
Sauti
1'41"
Photo Credit
UN News/Ziad Taleb