Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

UN Women: Wanawake Gaza hawataki kufa au kuzika wapendwa wao

UN Women: Wanawake Gaza hawataki kufa au kuzika wapendwa wao

Pakua

Baada ya ziara ya wiki moja huko Ukanda wa Gaza, Mashariki ya Kati, Maryse Guimond ambaye ni Mwakilishi Maalum wa shirika la Umoja wa Mataifa la masuala ya wanawake, UN Women katika eneo la Palestina linalokaliwa na Israeli,Israeli amesema kilicho alichoshuhudia hakina maelezo ya kutosha.

Akizungumza na waandishi wa habari mjini Geneva, Uswisi kutokea mjini Yerusalemu, Bi. Guimond amesema unapoingia tu kwenye kivuko cha Shalom na lango linafungwa, unahisi umefungiwa kwenye dunia ya uharibifu. Kuanzia shule, hospitali, makazi yaliyolundikana watu na uhaba wa vitu, watu wakihaha kusaka usalama, wanawake wakimuuliza vita itakoma lini? Na zaidi ya yote. 

“Wakazi wa Gaza wanataka hii vita ikome. Kila siku ambayo mzozo huu unaendelea, inazidi kuleta uharibifu na mauaji. Lazima hii ikome. Wavulana na wasichana walikuwa wananiuliza ni lini vita hii itaisha? Nami sikuwa na jibu la kuwapatia.” 

Akaendelea kusema.. 

“Gaza ni zaidi ya simulizi zaidi ya milioni mbili za kupoteza. Kila mwanamke niliyekutana naye ana simulizi ya kupoteza mtu. Zaidi ya wanawake 10,000 wamepoteza wapendwa wao. Zaidi ya familia 6,000 zimepoteza mama zao. Wanawake na wasichana milioni 1 wamepoteza utu wao, makazi yao, familia zao na kumbukumbu zao.” 

Bi. Guimond akasema kwa sasa..

"Swali si kwamba ni nini wanawake wanahitaji: Swali linapaswa kuwa ni nini wanawake hawahitaji. Wanawake hawataki kufa, hawataki kuzika wapendwa wao, hawataki kubakia wenyewe kupata machungu.”

Audio Credit
Assumpta Massoi
Audio Duration
2'14"
Photo Credit
WFP/Wissam Nassar