21 MEI 2024
Pakua
- Ripoti mpya iliyotolewa leo Mei 21 na Shirika la Umoja wa Mataifa la Afya Duniani, WHO inaashiria ongezeko kubwa la magonjwa ya zinaa duniani, huku kukiwa bado na changamoto za Virusi Vya Ukimwi na homa ya ini.
- Mkurugenzi Mkuu wa WHO, Dkt. Tedros Ghebreyesus kupitia ukurasa wake wa mtandao wa X ameeleza wasiwasi mkubwa walio nao juu ya usalama wa wagonjwa na wafanyakazi waliokwama katika hospitali ya Al-Awda kaskazini mwa Gaza.
- Shirika la Umoja wa Mataifa la Kuhudumia Wakimbizi (UNHCR) nchini Ukraine, limeeleza kuhusu wasiwasi mkubwa kutokana na hali inayozidi kuwa mbaya na kusababisha ongezeko la mahitaji ya kibinadamu kwa Waukraine na kulazimishwa kuyahama makazi yao kutokana na mashambulizi mapya ya ardhini ya Jeshi la Urusi katika eneo la kaskazini-mashariki la Kharkiv.
- Na katika mashinani leo tunakupeleka katika eneo Bunge la Ngong lililoko katika kaunti ya Kajiado nchini Kenya kusikia ujumbe kuhusu umuhimu wa utunzaji wa chemichemi ya maji.
Mwenyeji wako ni Flora Nducha, karibu!
Audio Credit
Flora Nducha
Audio Duration
10'52"