Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Walinda amani wa UN waweka doria kali mashariki mwa DRC baada ya kuibuka mapigano

Walinda amani wa Umoja wa Mataifa wanaohudumu kwenye ujumbe wa Umoja huo wa kulinda amani nchini DRC, MONUSCO wakiwa kwenye doria katika kijiji cha Logo mji wa Djugu jimboni Ituri .
MONUSCO

Amani na Usalama

Katika kukabiliana na hali ya mapigano makali yaliyoibuka tena mwishoni mwa wiki kati ya kundi lenye kujihami kwa silaha M23 na Jeshi la DR Congo (FARDC), walinda amani wa Umoja wa Mataifa kwa uratibu wa FARDC, wameweka doria karibu na Kanyabayonga kusaidia baadhi ya wanaume, wanawake na watoto 150,000 waliokimbia makazi yao katika siku za hivi karibuni mashariki mwa nchi.

Kupitia taarifa za mchana zake za mchana kwa waandishi wa habari, Msemaji wa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa amesema, “Walinda amani wa Umoja wa Mataifa wameripoti kwamba kumekuwa na mapigano makali kusini mwa Kanyabayonga katika eneo la Rutshuru la Kivu Kaskazini, mashariki mwa nchi.”

Mapigano hayo yalisababisha raia kuhama makazi yao kuelekea Kayna, Miriki na Kirumba, huku wengine wakifika Lubero na Butembo.

Vile vile, Msemaji wa Katibu Mkuu amesema, “mapigano makali pia yaliripotiwa katika siku chache zilizopita karibu na Sake. Ujumbe wa Umoja wa Mataifa wa kulinda amani nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo DRC, MONUSCO unafuatilia hali hiyo.”