Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Kasi ya kutoweka viumbe hai imesababisha athari kubwa ya upotevu wa bioanuwai: UN

Katika nyika za Kazakh, idadi ya saigas iliyowekwa kwenye orodha  nyekundu ya wanyama walio hatarini kupotea tayari imepita milioni 2.5.
Huduma ya vyombo vya habari ya Wizara ya Ikolojia na Maliasili ya Kazakhstan.
Katika nyika za Kazakh, idadi ya saigas iliyowekwa kwenye orodha nyekundu ya wanyama walio hatarini kupotea tayari imepita milioni 2.5.

Kasi ya kutoweka viumbe hai imesababisha athari kubwa ya upotevu wa bioanuwai: UN

Tabianchi na mazingira

Ijapokuwa karibu aina milioni moja ya viumbe hai kwa sasa ziko katika hatari ya kutoweka, Chuo Kikuu cha Umoja wa Mataifa UNU huko Bonn nchini Ujerumani kinatoa tahadhari ya "kutoweka kwa pamoja na athari zinazoingiliana zinatotokea wakati kuna kutoweka kabisa kwa aina moja kunakuathiri nyingine.

Suala hili linamulikwa leo pia katika Siku ya Kimataifa ya biolojia ya anuwai inayoadhimishwa kila mwaka tarehe 22 Mei, na kuangaziwa katika toleo la hivi karibuni zaidi la ripoti ya UNU ya hatari ya majanga yanayoingiliana.

Kwa mujibu wa ripoti hiyo miongoni mwa wanyama walio katika hatari ya kutoweka ni kobe aina ya gopher, mojawapo ya viumbe hai vya kale zaidi kwenye sayari dunia. 

Hadithi hii ya kusikitisha ya upotevu wa viumbe hai inajitokeza katikati mwa maeneo tambarare ya pwani ya kusini mwa Marekani.

Mfumo bunifu wa ikolojia 

Kupungua kwa idadi yao sio tu tatizo kwa maisha ya kobe kama aina ya viumbe hai, kwani viumbe hawa wenye haiba pia wana jukumu muhimu katika kuhifadhi usawa dhaifu wa ufalme wao wa pwani.

Kobe wa gopher sio wakaaji tu wa makazi yao  bali wao ni wasanifu majengo, wachongaji mazingira na kutoa hifadhi kwa zaidi ya viumbe vingine 350. Huku miguu yao ya mbele ikifanya kazi kama majembe, wanachimba mashimo yenye ukubwa wa futi 20 hadi 30  sawa na mita 6 hadi 9 na kina cha futi 6 hadi 8  sawa mita 1.8 hadi 2.5.

Kuanzia wadudu wadogo hadi viumbe maji au amfibia wakubwa, kila kiumbe kina jukumu muhimu katika mfumo tata wa maisha wa mashimo haya. Kwa wengine, mashimo ya kobe wa gopher ni mahali salama pa kuzaliana na kulea watoto, wakati kwa wengine, hutoa maficho kutoka kwa wanyama wanaowinda wanyama wengine na vitu.

Iwapo kobe wa gopher atatoweka, kuna uwezekano athari yake itasikika katika mfumo wote wa ikolojia.

Pia Umoja wa Mataifa umetaja viumbe wengine walio hatarini kutoweka miongoni ni chura aina ya dusky gopher, aina ambayo tayari iko kwenye ukingo wa kutoweka. 

Kwa kutegemea mashimo ya kobe kwa ajili ya makazi na kuishi, kutoweka kwa kobe kunaweza kuweka maisha ya chura katika hatari pia.

Kisiwa cha Fogo huko Cabo Verde kiliteuliwa kama hifadhi ya viumbe hai mnamo 2020.
© UNDP/Projecto Vitó Association
Kisiwa cha Fogo huko Cabo Verde kiliteuliwa kama hifadhi ya viumbe hai mnamo 2020.

Jukumu la wanadamu

Katika kuangazia zaidi juu ya kutoweka kwa pamoja, UNU imesema kuwa shughuli kubwa za binadamu, kama vile mabadiliko ya matumizi ya ardhi, matumizi ya kupita kiasi, mabadiliko ya hali ya tabianchi, uchafuzi wa mazingira na kuanzishwa kwa viumbe vamizi, vinasababisha kasi ya kutoweka viumbe ambayo ni angalau mara kumi hadi mamia haraka kuliko mchakato wa asili wa kutoweka kwa viumbe.

Katika miaka 100 iliyopita, kwa mfano zaidi ya aina 400 za wanyama wenye uti wa mgongo zilipotea. 

Kwa hivyo ripoti hiyo inajumuisha kutoweka kwa kasi kati ya pointi zake 6 za hatari zilizounganishwa.

Hoja kama hizo hufikiwa wakati mifumo ambayo binadamu hutegemea haiwezi kuzuia hatari na kuacha kufanya kazi kama inavyotarajiwa haswa kama matokeo ya vitendo vya wanadamu.

Kutoweka huzaa kutoweka

Ripoti inasema mifumo ya ikolojia imejengwa juu ya mitandao tata ya muunganisho kati ya aina tofauti, kama mfano wa chura wa gopher, kobe-dusky unavyoonyesha.

Athari ya kutoweka inaweza kusababisha aina nyingi kutoweka na hatimaye hata kuporomoka kwa mfumo mzima wa ikolojia.

Kwa kuwa karibu aina milioni moja za mimea na wanyama ziko hatarini kwa sasa, athari mbaya ya kutoweka kwa aina moja inaweza kuathiri wengine wengi, na kuvuruga utendaji muhimu wa ikolojia.

Siri wa bahari walio hatarini kutoweka ni mfano mwingine wa utegemezi tata ndani ya mifumo ikolojia. 

Wakiita misitu ya kelp ya Pasifiki kuwa makazi yao, hapo awali ilikuwa mingi, lakini sasa iko hatarini kutoweka ndani ya nchi kwa sababu ya kuwindwa bila kuchoka kwa manyoya yao hapo awali.

Katika mifumo iliyopangwa vizuri ya kiikolojia, simba wa baharini huwinda nyangumi wa baharini, na hivyo kusimamisha ukuaji usiozuiliwa wa idadi ya wanyama wa baharini. 

Bila kuwepo kwa mnyama aina ya siri malisho haya yenye miiba hukimbia sana, na hivyo kubadilisha misitu yenye majani mabichi ya mikuyu.

Lakini kuangamia kwa samaki wa baharini kunaweza kuwa na athari ambazo zinaenea zaidi ya kutoweka kwa kelp pekee, UNU imesema. 

Zaidi ya aina 1,000 ikiwa ni pamoja na papa, kasa, siri, nyangumi, ndege, na wingi wa samaki hutegemea maeneo haya ya chini ya maji kwa kuwepo kwao.

Misitu hufunika 93% ya ardhi ya Suriname na ina wingi wa viumbe hai.
UNDP Suriname/Pelu Vidal
Misitu hufunika 93% ya ardhi ya Suriname na ina wingi wa viumbe hai.

Kuunda mustakbali tunaoutaka

Kushughulikia mzozo wa bioanuwai kunahitaji mbinu mbalimbali zinazotambua muunganiko wa hatari na suluhu.

Kaulimbiu ya Siku ya Kimataifa ya biolojia ya anuwai inatoa wito kwa kila mtu kuunga mkono utekelezaji wa Mpango wa Bioanuwai, uliopitishwa mwaka 2022, ambao unaweka malengo na hatua madhubuti za kukomesha na kurudisha nyuma upotevu wa asili ifikapo 2050.

Moja ya malengo ni pamoja na kupunguza kiwango cha kutoweka kwa viumbe vyote mara kumi hadi katikati ya karne hii na kuongeza wingi wa wanyamapori wa asili hadi viwango vya afya na umnepo, amesema Zita Sebesvari, Naibu Mkurugenzi wa Taasisi ya UNU ya Mazingira na Usalama wa Binadamu na mwandishi mkuu wa Ripoti ya Hatari za Maafa Zilizounganika.

Ameeleza kuwa "Wakati mikakati ya kukabiliana na hali hiyo, kama vile kurejesha na kulinda njia za kuhifadhi mazingira kati ya makazi ya wanyama hutoa ahueni, kukabiliana na vichochezi vya kutoweka ambayo bado ni muhimu, kwa sababu lengo hili haliwezi kufikiwa wakati bado tunahatarisha kuharakisha kutoweka kwa viumbe."

Kwa muda mrefu, kuepuka kutoweka na kutoweka kwa pamoja kutakuwa suluhisho pekee la kweli la kukomesha upotevu wa bayoanuwai, ambayo inahitaji mabadiliko ya mawazo.

"Juhudi za uhifadhi lazima zienee zaidi ya aina za kibinafsi ili kujumuisha mfumo mzima wa ikolojia", amesema Bi. Sebesvari.

Ameongeza kuwa "Hatua za haraka na madhubuti zinahitajika ili kuhifadhi uthabiti wa mifumo ya ikolojia na kuhakikisha uhai wa mitandao mbalimbali ya maisha ya sayari yetu. Kukumbatia asili kama sehemu muhimu ya utamaduni wetu ni muhimu ili kupata mustakabali endelevu, kwa kutambua kwamba hatima yetu inafungamana na hatima ya ulimwengu wa asili.”