Ninajisikia fahari sana kutatua changamoto za wanawake na watoto wa CAR - Meja Lilian Laizer
Ninajisikia fahari sana kutatua changamoto za wanawake na watoto wa CAR - Meja Lilian Laizer
Amani na Usalama
Makala hii inamwangazia Meja Lilian Laizer, Mlinda amani wa Umoja wa Mataifa anayehudumu katika Kikosi cha 7 cha ulinzi wa amani kutoka Tanzania TANBAT 7 kinachohudumu nchini Jamhuri ya Afrika ya Kati, CAR chini ya MINUSCA ambao ni Ujumbe wa Umoja wa Mataifa wa Kulinda amani nchini humo.
Meja Lilian Laizer anashughulika na masuala ya jinsia na watoto katika kikosi na jamii ya wenyeji.