Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Azimio la 5 la Manama lapitishwa, watu wenye ulemavu waonesha ubingwa wao kwenye ugunduzi

Kundi la watu wenye ulemavu ambao wanashiriki Jukwaa la WEIF 2024
UN News/Abdelmonem Makki
Kundi la watu wenye ulemavu ambao wanashiriki Jukwaa la WEIF 2024

Azimio la 5 la Manama lapitishwa, watu wenye ulemavu waonesha ubingwa wao kwenye ugunduzi

Ukuaji wa Kiuchumi

Azimio la 5 la Manama limepitishwa hii leo huko Manama, mji mkuu wa Bahrain na washiriki wa Jukwaa la Kimataifa la Uwekezaji kwa Wajasiriamali likiwa na wito wa pamoja na mambo mengine  likisihi jamii ya kimataifa na wadau wote katika sekta ya umma na binafsi kutumia nguvu ya ujasiriamali na uwekezaji katika nyanja zote za kiuchumi na kijamii kama kitovu cha kufanikisha Malengo ya Maendeleo Endelevu, SDGs kwa kupatia kipaumbele makundi maalum wakiwemo watu wenye ulemavu, wanawake, vijana na familia zinazohaha kutumia uwezo wa kuzalisha ili kujikimu kimaisha.

Jukwaa hili linaratibiwa na shirika la Umoja wa Mataifa la maendeleo ya viwanda, UNIDO ofisi ya Kusongesha Ugunduzi na Teknolojia, ITPO nchini Bahrain na kufadhiliwa na wadau wa kitaifa, kikanda na kimataifa.

Hoja ya ugunduzi na ujasiriamali kama njia mojawapo ya kufanikisha SDGs imedhihirika kando ya mkutano huo ambako watu wenye ulemavu wa aina mbalimbali wamedhihirisha ni kwa jinsi gani teknolojia inawasaidia kuruka vikwazo na hatimaye kujenga jamii jumuishi, moja ya wito aliotoa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres kupitia taarifa yake iliyowasilishwa kwenye jukwaa hilo.

“Tunapotazamia mkutano wa zama zijazo mwezi Septemba, nahamasisha jukwaa hili kusaka mbinu za kutumia uwezo wa ujasiriamali na ugunduzi ili dunia yetu iwe pahala bora kwa wakazi wote wa sayari hii tunayotumia pamoja,” amesema Katibu Mkuu.

Dkt. Hashim Hussein, Mkuu wa UNIDO/ITPO Bahrain anasema kwamba suala la matumizi ya ugunduzi na ujasiriamali kwa ajili ya kusongesha SDGs na ujumuishi kwenye jamii ni muhimu sana duniani akitolea mfano nchi za kiarabu ambako asilimia 15 ya watu wana ulemavu.

Assumpta Massoi wa UN News akimuhoji Olfa Dabbabi mwanamke kutoka Tuniasia ambaye alianzisha kampuni ya OLFUS, inayotumia sanaa ya kidijitali kuwasilisha ujumbe mbalimbali, ikiwa ni pamoja na kuwatia moyo watu wanaokabiliwa na cbi, a young womhallenges.
UN News/Abdelmonem Makki
Assumpta Massoi wa UN News akimuhoji Olfa Dabbabi mwanamke kutoka Tuniasia ambaye alianzisha kampuni ya OLFUS, inayotumia sanaa ya kidijitali kuwasilisha ujumbe mbalimbali, ikiwa ni pamoja na kuwatia moyo watu wanaokabiliwa na cbi, a young womhallenges.

Watu wenye ulemavu na teknolojia WEIF2024

Miongoni mwa watu wenye ulemavu walioonesha uthabiti wa teknolojia na ugunduzi katika kujenga jamii jumuishi ni Olfa Dabbabi, msichana kutoka Tunisia ambaye hakukubali changamoto ya ulemavu alionao kumnyima haki ya kusaidia jamii yake hasa wakati huu ambapo dunia imegubikwa na uonevu wa mitandaoni na watu kusemwa vibaya kutokana na mionekano ya miili yao.

“Mimi nina ulemavu kwenye mfumo wa mishipa ya fahamu au neva,” amesema Olfa akizungumza na Idhaa ya Umoja wa Mataifa kwenye kibanda cha kuonesha kazi zake za sanaa za kidijitali akiongeza kuwa “hata kama nina ulemavu niliozaliwa nao haikunikwamisha bali ulinichochea kukabiliana nao na kuwa mwanamke niliye sasa. Ugunduzi na teknolojia sio tu jambo ninalopenda bali ni jambo linaloniwezesha kufanya kazi ninayofanya sasa.

Olfa ameanzisha kampuni iitwayo Olfus ambayo inatumia sanaa za kidijitali kupeleka ujumbe mbali mbali ikiwemo kuwatia watu moyo walio na changamoto akisema, “napenda kuzungumzia uonevu kwa sababu sio jambo jema kufanya. Nazungumzia pia umuhimu wa kujikubali tulivyo, na kukataa kukataa kauli mbayá dhidi ya miili ya watu na pia kuhusu afya ya akili. Mimi mwenyewe nilikumbwa na uonevu nikiwa mdogo, niña ulemavu na ndio hapo nilikumwba na uonevu, lakini familia yangu ilikuwa nami.”

Nadia Musleh ni Rais wa jumuiya ya Renaissance ya Wanawake huko Ramallah, ambacho kilianzishwa mwaka 1925.
UN News/Abdelmonem Makki
Nadia Musleh ni Rais wa jumuiya ya Renaissance ya Wanawake huko Ramallah, ambacho kilianzishwa mwaka 1925.

Taswira ya matumaini Palestina

Nadia Musleh ni Rais wa Jumuiya ya Renaissance ya Wanawake huko Ramallah, ambacho iliyoanzishwa mwaka 1925.

“Chama kilianzisha mradi wa kwanza wa kuhudumia watu wenye ulemavu nchini Palestina mwaka 1972, kuwapatia elimu na matunzo. Tuna kituo cha kurekebisha tabia ambacho huhudumia walemavu kati ya 45 na 60 kila siku. Tunawapa mipango na programu za kila siku. Kituo hicho kinafundisha watu wenye ulemavu jinsi ya kutengeneza zana mbalimbali za mikono, pamoja na kupaka rangi na kuchora. Tulikuja hapa kuangazia tulichonacho Palestina,” amesema Nadia Musleh alipozungumza na UN News.

Pia ameongeza kuwa "Pamoja nasi ni Anton, ambaye alijiunga na chama akiwa na umri wa miaka 3. Sasa ana umri wa miaka 40 na amebobea katika kuandaa baadhi ya michezo.” 

Kukumbatia sekta mpya kama vile uchumi bunifu wa rangi ya chungwa

Azimio la Manama pia linatoa wito kwa jumuiya ya kimataifa kukuza na kutumia sekta mpya zenye matumaini kama vile uchumi wa ubunifu wa chungwa, kukumbatia mageuzi ya kidijitali, ikiwa ni pamoja na akili mnemba, na kusisitiza mbinu za kilimo bora ambazo zitaunda nafasi zaajira na kufikia maendeleo ya kiuchumi.

Serikali, sekta binafsi, wanazuoni, mashirika ya kiraia, vyombo vya habari na mashirika ya kimataifa, pamoja na waendeshaji wote wa mfumo wa ikolojia, wametakiwa kushirikiana katika kuwezesha uendelezaji wa ujasiriamali na makampuni ya ubunifu ili kufikia Malengo ya Maendeleo Endelevu na mtazamo wa kuelekea mwaka 2050.

Waraka huo wa kurasa mbili, ambao pia utawasilishwa kwenye Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa, unamalizia kwa wito kwa jumuiya ya kimataifa "kumaliza migogoro na kutoa msaada wa haraka kwa wanawake na vijana katika maeneo yenye migogoro baada ya migogoro hiyo."

Jukwaa hilo la siku tatu litakamilika kesho likilenga zaidi wanawake, amani na usalama, jinsi ya kukuza utulivu katika nchi zilizoathiriwa na migogoro kwa kufadhili wajasiriamali wa kike.

Olfa anasema anatumia teknolojia ya kompyua na Akili Mnemba kutengeneza sanaa zake na kusaidia wale wanaokumbwa na changamoto kama alizokumbana nazo akisema kadri siku zinavyosonga tunahitaji Akili Mnemba zaidi na zaidi.

Abdullah Shabana kutoka Saudia amekuja na wazo la mfumo wa ushirikishwaji ulioanzishwa na MIT na mamlaka ya Saudia kwa ajili ya haki miliki
UN News/Abdelmonem Makki
Abdullah Shabana kutoka Saudia amekuja na wazo la mfumo wa ushirikishwaji ulioanzishwa na MIT na mamlaka ya Saudia kwa ajili ya haki miliki

“Kujenga madaraja”

Abdullah Shabana kutoka Saudi Arabi ana wazo lake la ubunifu jumuishi, wazo ambalo lilianzishwa na Chuo Kikuu cha teknolojia cha MIT nchini Marekani na Mamlaka ya Haki miliki ya Saudi Arabia.

“Ubunifu shirikishi ni mpango ambao unaleta pamoja wabunifu na watu wenye ulemavu, ambapo wanashirikiana kufanikisha jambo muhimu, kuanzia utafiti waw azo hadi utekelezaji na kupitia ubunifu jumuishi, miradi mingi zaidi inabuniwa,” amesema Abdullah akizungumza na Idhaa ya Umoja wa Mataifa.

“Mradi ambao tunawasilisha leo ni matumizi ya sauti, ambayo matumizi yake yanalenga kusaidia watu wenye changamoto za mawasiliano, kwani apu hiyo inasaidia wenye changamoto za mawasiliano kuwasiliana na wenzao.”

Zaidi kutoka azimio la Manama 5

Azimio la Manama pia linataka jamii ya kimataifa iendeleze na kujinufaisha na sekta mpya zinazotia matumaini kama vile sekta ya ubunifu au Orange Economy, mabadilko ya kidijitali ikiwemo akili mnemba na kujumuisha kilimo janja ambacho kitaongeza fursa za ajira na hivyo kusongesha maendeleo.

Serikali, sekta binafsi, Vyuo Vikuu, mashirika ya kiraia, vyombo vya habari, mashirika ya kiraia na wahisani washirikiane ili kusongesha ujasiriamali na kampuni za ugunduzi ili kufanikisha SDGs.

Dkt. Hashim Hussein (kwenye skrini) Mkuu wa UNIDO/ITPO ofisi ya Bahrain akiwasilisha Azimio la Manama wakati wa WEIF 2024
UN News/Abdelmonem Makki
Dkt. Hashim Hussein (kwenye skrini) Mkuu wa UNIDO/ITPO ofisi ya Bahrain akiwasilisha Azimio la Manama wakati wa WEIF 2024

Azimio hilo pia litakalowasilishwa Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa linataka pia jamii ya kimataifa imalize mizozo na kusaidia wanawake na vijana kwenye maeneo ambako mizozo imemalizika.

Jukwaa hili la siku tatu linatamatika kesho Alhamisi likiwa na mada lukuki ikiwemo ile ya Wanawake na amani na usalama, uwezeshaji wa wanawake wajasiriamali kwenye maeneo yenye mizozo.